Kitengo cha maarifa ya kiislamu na kibinadamu chini ya Atabatu Abbasiyya tukufu, kinaendelea kufanya semina kwa watumishi wake, na sasa kinaendesha semina ya (Bibliography) kwa ajili ya kuwajuza watumishi na kuwajengea uwezo katika sekta hiyo, hasa idara ya utunzaji wa taarifa kutokana na umuhimu wa vipengele vinavyo hitajiwa kama vile (faharasi, usanifu na uhakika wa njia zake).
Mkufunzi wa semina hiyo alikua ni Ustadh Hassan Aribiy Khalidi, kwa mujibu wa maelezo yake amesema kua: “Kulikua na vipengele vingi, wamefundishwa (kwa nadhariyya na vitendo), wamepewa maelezo na ufafanuzi kuhusu Program hiyo na maneno yanayo tumika kwa lugha ya kiengereza kama yanavyo tumiwa duniani kote, pamoja na ufafanuzi wa kina kuhusu vigawanyo vyake sambamba na kuelezea faida za (Bibliography)”.
Akasisitiza kua: “Nimeona uwepo wa matashi ya kweli ya washiriki katika semina hii, yaliyo wawezesha kuelewa kwa haraka, kwa hakika mjuzi wa program hii humrahisishia mtu kutafuta anacho hitaji kwa urahisi”.
Naye kiongozi wa idara ya utunzaji wa taarifa Amjadi Barqaáwi amesema kua: “Kutokana na kuongezeka kwa elimu na kupanuka kwa program, mtafiti anahitaji muda mrefu kupata taarifa fulani, atatumia muda mwingi na nguvu kubwa, lakini kwa kutumia program ya (Bibliography) kazi huwa rahisi na fupi, baada ya kuwekwa faharasi ya tafiti na vitabu pamoja na majina ya waandishi na vinginevyo ambayo hutumika katika program ya (Bibliography)”.