Ofisi ya maadhimisho ya matukio ya kidini chini ya idara ya masayyid wanaofanya kazi katika Atabatu Abbasiyya tukufu, ikiwa kama sehemu ya ratiba ya kuomboleza msiba huu mchungu, wamefanya majlis ya kuomboleza kifo cha Imamu Zainul-Abidiina Ali bun Hussein (a.s), asubuhi ya Alkhamisi (26 Muharam 1441h) sawa na (26 Septemba 2019m) ndani ya ukumbi wa haram ya Abulfadhil Abbasi (a.s) na kuhudhuriwa na idadi kubwa ya mazuwaru.
Shekh Ali Mujaan kutoka kitengo cha Dini katika Atabatu Abbasiyya tukufu amepanda mimbari na akaeleza maisha ya Imamu Zainul-Abidiina (a.s), kwa kufafanua hatua mbalimbali za uhai wake (a.s), hasa baada ya vita ya Twafu, namna alivyo eneza fikra za Imamu Hussein na kupambana na fikra za Umawiyya, na jinsi alivyo simama kidete kuendeleza mwenendo wa Islahi ulio simamiwa na baba yake bwana wa mashahidi (a.s) na kuyafanya mapinduzi ya Husseiniyya kuendelea kua hai, na kulea kizazi kipya cha waislamu wanao fuata nyayo za Imamu Hussein (a.s), pia aliongelea sekta ya ibada katika uhai wa Imamu Zainul-Abidiina (a.s), yeye ndiye aliyepewa jina la laqabu (sifa) la Sayyid Saajidiina (bwana wa wasujudio), alijulikana kwa uchamungu wake na ukarimu wake kwa watu na jinsi alivyokua akiwasaidia mafakiri.
Majlis ikahitimishwa kwa kaswida na tenzi za kuomboleza zilizo anyesha ukubwa wa msiba wa kifo cha Imamu wa nne Ali bun Hussein (a.s).
Fahamu kua idara ya Masayyid wanaofanya kazi katika Atabatu Abbasiyya katika kila tukio la kukumbuka kifo cha Imamu Maasum hufanya majlis ya kuomboleza ndani ya ukumbi wa haram ya Abulfadhil Abbasi (a.s).