Kitengo cha uwanja wa katikati ya haram mbili tukufu chavuna kilo (7500) za tende na kuziweka katika vifurushi kwa ajili ya kuzigawa bure kwa mazuwaru

Maoni katika picha
Idara ya miti na mapambo katika kitengo cha eneo la uwanja wa katikati ya haram mbili tukufu Husseiniyya na Abbasiyya, kimevuna tende zilizopo katika uwanja huo mtukufu pembezoni mwa eneo lililopauliwa, kwa ajili ya kuzigawa kwa mazuwaru kama zawadi ya kutabaruku, kiasi cha kilo (7500) zimewekwa kwenye vifungashio kwa jina la kitengo hicho.

Kiongozi wa idara ya miti na mapambo katika kitengo cha uwanja wa katikati ya haram mbili tukufu, Mhandisi Haatim Abdulkarim Habibu ameuambia mtandao wa Alkafeel kua: “Miti ya tende inatengeneza mazingira mazuri ya kijani kibichi katika eneo hili, jambo lililo sababisha uongozi wa kitengo kuweka mfumo maalum wa umwagiliaji na kutafuta pembejeo bora kabisa za kilimo, sambamba na kubadilisha baadhi ya miti ya mitende na kupanda aina adim, kwa ajili ya kufanikisha kupata mavuno makubwa yanayo kadiriwa kua zaidi ya tani saba, na kuzigawa kwa mazuwaru baada ya kuzichambua na kuziweka kwenye vifungashio vyenye ujazo wa (gram 750) kwa jina la kitengo hicho, kisha kuzigawa bure kwa mazuwaru”.

Akaongeza kua: “Tumepanga siku ya Alkhamisi na usiku wa Ijumaa kua siku za kugawa tende hizo kwa ajili ya kuwafikia idadi kubwa zaidi ya mazuwaru, kwani siku hiyo huwa na mazuwaru wengi tofauti na siku zingine, mazuwaru hao wanatoka ndani na nje ya Iraq, zowezi hilo limepata mwitikio mkubwa na shukrani nyingi kutoka kwa mazuwaru”.

Kumbuka kua idara ya miti na mapambo chini ya kitengo cha eneo la uwanja wa katikati ya haram mbili tukufu, inafanya juhudi ya kutunza bustani iliyopo kwenye eneo hilo hasa mitende, kwa kupanda aina adim za tende na kuiwekea bembejeo bora zaidi kwa ajili ya kuongeza mavuno.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: