Vipengele muhimu alivyo ongea Marjaa Dini mkuu katika khutuba ya swala ya Ijumaa

Maoni katika picha
Marjaa Dini mkuu katika khutuba ya pili ya swala ya Ijumaa iliyo swaliwa ndani ya haram ya Imamu Hussein (a.s) leo (27 Muharam 1441h) sawa na (27 Septemba 2019m), chini ya uimamu wa Mheshimiwa Shekh Abdulmahdi Karbalai, ameongea vipengele vingi vya kimaadili na kimalezi vinavyo endana na mazingira halisi tunayo ishi kwa sasa, amesisitiza zaidi umuhimu wa kunufaika na Risalatul Huquuq ya Imamu Sajjaad (a.s) na kuifanyia kazi kwa vitendo, miongoni mwa aliyo sema ni:

  • - Risalatul Huquuq ni miongoni mwa hazina za maarifa ya Mwenyezi Mungu, ambayo tumegharilika kutambua umuhimu wake katika maisha ya duniani na akhera.
  • - Risalatul Huquuq ni miongoni mwa hazina muhmu za maarifa ya Mwenyezi Mungu, sio kwamba tunatakiwa kujifunza tu bali tunatakiwa kuyafanyia kazi yaliyomo.
  • - Risalatul Huquuq inazungumzia haki zote za binadamu ni bahari inayo hitajiwa na kila mtu, kiongozi, raia, mchunga na mchungwa.
  • - Miongoni mwa vitu muhimu katika kuhuisha kumbukumbu za Maimamu (a.s) ni kufanya majlis za kuelezea elimu zao.
  • - Tunasoma na kusomesha elimu zao pamoja na kuzifanyia kazi kwa vitendo.
  • - Kama tukiangalia kwa undani sababu za mizozo yetu tutakuta ni matokeo ya kutoheshimu haki za watu.
  • - Kila siku mtu hupigania haki zake kwa watu wengine lakini yeye hatekelezi haki za wengine.
  • - Kila mtu anataka Mwenyezi Mungu ampe kila kitu, lakini yeye anatekeleza mambo anayo taka Mwenyezi Mungu kwake?!
  • - Kila mtu anatakiwa aheshimu haki za watu wengine.
  • - Watoto wanataka wazazi wao wawape haki zao, je wao wanawapa wazazi haki zao?!
  • - Mtu anataka jamii itende haki, je yeye anaitendea kahi jamii?
  • - Jambo kubwa la msingi kila mtu huwataka watu watende haki wakati yeye hatendi haki.
  • - Tunatakiwa kuzingatia japo baadhi ya mambo katika Risalatul Huquuq ya Imamu Sajjaad (a.s).
  • - Tunatakiwa kuifundisha Risalatul Huquuq katika shule zetu, vyuo vyetu, taasisi zetu, kwenye familia zetu na kila mahala.
  • - Tunatakiwa kuzungumzia haki hizo katika majlis za Husseiniyya na kuwatambulisha watu Risaralul Huquuq kitabu ambacho kimeandika haki zote za mwanadamu na mazingira yanayo mzunguka.
  • - Imamu Zainul-Abidina (a.s) katika kitabu hicho amefafanua haki za kuishi kijamii kuanzia ndani ya familia.
  • - Imamu Zainul-Abidina (a.s) amefafanua haki ya mume kwa mkewe na haki za mke kwa mumewe na haki za wazazi.
  • - Siku hizi tunashuhudia uvunjifu wa haki za wazazi, haki za baba na mama.
  • - Uwepo ni neema kubwa kwa mwanadamu, kaumbwa na Mwenyezi Mungu mtukufu na kapewa neema ya uwepo, tunakusudia malezi ya kimwili na kiakili.
  • - Baba ndio msingi wa neema ya uwepo na malezi kumfanyia wema ni jambo muhimu kwako ewe kijana ole wako usipo mtendea wema.
  • - Mama alipata matatizo mengi kwa ajili yako, matatizo ambao hakuna mtu mwingine yeyote anayeweza kuyavumilia duniani kwa sababu yako.
  • - Ole wako usiache kuwafanyia wema wazazi wako uwe utakavyo kua.
  • - Lazima ukumbuke asili ya neema ya uwepo na malezi yaliyo kufikisha hapo, bila shaka shukrani zinararudi kwa baba na mama.
  • - Usisahau wema wao kwako kutokana na mali au madaraka uliyo nayo.
  • - Kama unavyo taka wazazi wako wakutendee haki unatakiwa pia na wewe uwatendee haki.
  • - Ustadhi na mwalimu wamefanywa kua hazina ya elimu na wana haki zao, pia wao wanatakiwa watekeleze haki ya elimu.
  • - Asifikiri yeyote kua kutokana na juhudi au ujanja wake peke yake ndio umemfikisha hapo alipo, bali Mwenyezi Mungu mtukufu kakupa uwelewa na kakutengenezea mazingira na kukufanya kuwa hazina ya elimu.
  • - Elimu ni amana kwako unatakiwa kuifikisha kwa wengine.
  • - Ustadhi alikua na ustadhi aliye mfundisha na mwalimu alikua na mwalimu aliye mfundisha na wewe ni jukumu lako kufundisha.
  • - Ustadhi na mwalimu wanawajibika kufiksha elimu waliyo fundishwa kwa wengine ikiwa salama na sahihi.
  • - Ustadhi na mwalimu wanatakiwa kua na subira safari ya elimu ni ngumu na inahitaji kuendelea.
  • - Elimu bila adabu na maadili mema haina faida.. hubadilika na kua hatari kwa mwenye nayo na jamii.
  • - Tunatakiwa kufikisha mada za masomo kwa uwazi kwa usahihi katika akili ya mwanafunzi na kumpa malezi bora yatakayo mfanya kua na tabia nzuri.
  • - Tunatakiwa kufanya kila tuwezalo katika kumfundisha mwanafunzi tabia nzuri sambamba na elimu.
  • - Kama tukiwapa elimu bila tabia njema watapotea.
  • - Tunatarajia taasisi zote za elimu zijikite katika mambo mawili makubwa, elimu na malezi bora.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: