Vituo mbalimbali vya taaluma na ufundi: Jumuiya ya Skaut Alkafeel yafungua maonyesho ya nne

Maoni katika picha
Katika kumbukumbu ambayo hufanywa kila mwaka ya kubomolewa kwa kubba la maimamu wawili Askariyyain (a.s) na katika ratiba ya (Labbaika yaa Hussein/3), siku ya Ijumaa (27 Muharam 1441h) sawa na (27 Septemba 2019m) chini ya eneo lililo pauliwa ndani ya uwanja wa katikati ya haram mbili tukufu, Jumuiya ya Skaut Alkafeel chini ya idara ya watoto na makuzi imefanya maonyesho ya nne yatakayo dumu kwa muda wa siku tatu, hafla ya ufunguzi wa maonyesho hayo imehudhuriwa na viongozi wa idara pamoja na mazuwaru.

Kwa mujibu wa wasimamizi wa maonyesho hayo, yanahusisha vitu vingi, kikiwepo kituo maalum cha utowaji wa huduma za kwanza za uokozi, katika kujiandaa na kuokoa mtu yeyote atakaye patwa na tatizo la iana yeyote kwenye ziara ya Arubaini, sambamba na mabango maalum yaliyo andikwa ujumbe unaohusu mapinduzi ya Imamu Hussein (a.s).

Upande wa wanahabari kulikua na picha za matukio mbalimbali, pamoja na fikra zilizo andikwa kiubunifu, pia katika maonyesho haya kuna michoro ya aina mbalimbali, na tawi maalum kwa ajili ya kuonyesha harakati za jumuiya ya Skaut ya Alkafeel na ushiriki wao wa mwisho katika shughuli za nje.

Kumbuka kua kazi za mikono zilizo onyeshwa zimefanywa na wanaskaut ispokua baadhi ya picha, zimetokana na kamera za idara ya picha na uzalishaji chini ya kitengo cha habari na utamaduni cha Ataba tukufu.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: