Kwa nini leo mawakibu za watu wa Hilla zimekwenda katika malalo ya Imamu Hussein na ndugu yake Abulfadhil Abbasi (a.s)?

Maoni katika picha
Kwa sababu wao ndio watu wa mwisho kuwaaga mazuwaru wanaokwenda kwa miguu katika ziara ya Arubaini, na wao wanaishi katika mji uliokirimiwa na Mwenyezi Mungu kwa kua karibu na mkoa mtukufu wa Karbala, na kuufanya kua mji unaokanyagwa na miguu ya mazuwaru wa Imamu Hussein (a.s), baada ya kufungamana jina lake na jina la Imamu Hassan Almujtaba (a.s), na hili linaonekana katika mawakibu zao na kua ni kiigizo kwa mawakibu za mikoa mingine.

Watu wa mji huo huwahudumia mazuwaru katika msimu wote wa ziara ya Arubaini, baada ya Adhuhuri ya leo (27 Muharam 1441h) sawa na (27 Septemba 2019m) mawakibu za kuomboleza (za matam na zanjiil) zimeanza matembezi kutoka vitongoji tofauti vya mkoa wa Baabil, kwa ajili ya kuhuisha maombolezo matukufu ya Husseiniyya waliyo zowea kuyafanya katika siku kama hizi, huanza kuelekea katika malalo mbili tukufu baada ya kumbukumbu ya kifo cha Imamu Sajjaad (a.s), kila maukibu hufuata ratiba maalum iliyo pangiwa na kitengo cha maadhimisho na mawakibu Husseiniyya katika Ataba mbili tukufu Husseiniyya na Abbasiyya.

Kuwasili kwa mawakibu hizo kwa mujibu wa maelezo ya rais wa kitengo cha maadhimsho na mawakibu Husseiniyya katika Ataba mbili tukufu bwana Riyaadh Niámah Salmaan kuna sababu mbili: “Kwanza ni kwa ajili ya kuomboleza kifo cha Imamu Sajjaad (a.s), pili asilimia kubwa ya mawakibu hizo zinafanya kazi ya kuhudumia mazuwaru wanaotembea kwenda kwenye ziara ya Arubaini ya Imamu Hussein (a.s), hawawezi kuja Karbala na kushirikiana na mawakibu zingine katika siku za ziara ya Arubaini, imekua desturi yao kufanya hivi kwa miaka mingi”.

Akaongeza kua: Idadi ya maukibu hizo ni zaidi ya (86), matembezi yao yameanzia barabara ya Kibla ya Abulfadhil Abbasi (a.s) kuelekea katika haram yake kutufu kisha zinaenda kwenye malalo ya Abu Abdillahi Hussein (a.s) kwa kupitia kwenye uwanja wa katikati ya haram mbili na kuhitimisha maombolezo yao ndani ya malalo ya Abu Abdillahi Hussein (a.s), chini ya usimamizi wa watumishi wa Ataba hizo katika kuratibu na kusimamia matembezi hayo ili yasitatize mazuwaru watukufu.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: