Kituo cha ukarabati wa nakala kale: Chakarabati msahafu wa kihistoria wenye zaidi ya miaka (200)

Maoni katika picha
Kituo cha ukarabati wa nakala kale chini ya maktaba na Daru Makhtutwaat ya Atabatu Abbasiyya tukufu, hivi karibuni kimekamilisha ukarabati wa msahafu wa kihistoria wa karne ya kumi na mbili hijiriyya, nao ni katika mali za msikiti wa Shekh Tusi (r.a) katika mkoa wa Najafu, msikiti huo una nakala kale adimu ukiwemo msahafu huo wa kihistoria, kwa ajili ya kuuhifadhi, kutokana na kuishi miaka mingi karatasi zake zilikua zimeharibika, umekarabatiwa kwa kutumia njia za kisasa zaidi na umekua na muonekano mpya.

Mkuu wa kituo Ustadh Liith Ali Hussein ameuambia mtandao wa Alkafeel kua: “Kutokana na kauli ya kiongozi wa waumini Ali bun Abu Twalib (a.s) isemayo kua: (Zaka ya elimu ni kuifundisha) kwa lengo la kusaidiana na kubadilishana uzowefu kati ya kituo chetu na taasisi zingine za maktaba, mafundi wa kituo chetu wamefanya kazi ya kukarabati msahafu huo kama sehemu ya muendelezo wa kazi za aina hiyo wanazo fanya ndani na nje ya Atabatu Abbasiyya tukufu kwa ajili ya kudumisha turathi na nakala kale adimu na kuzilinda zisiharibike”.

Akaongeza kua: “Msahafu huu umekarabatiwa kwa kutumia njia za kisasa zaidi zinazo tumika katika fani hii duniani, zimeondolewa dosari zote zilizo kuwepo kwenye karatasi zake kwa umakini wa hali ya juu, bila kuathiri maandishi na muonekano wake, baada ya kufanya upembuzi yakinifu kuhusu uharibufu uliopo kwenye msahafu huo tukaanza kazi ya kuukarabati, tumekamilisha kazi hiyo kwa muda uliopangwa sambamba na kutunza nakala hiyo kwenye kompyuta kwa ajili ya kuuhifadhi”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: