Ilitokea siku kama ya leo mwezi mosi Safar mwaka 61h: Kuwasili mateka wa msafara wa Imamu Hussein (a.s) pamoja na kichwa chake kitakatifu huko Sham

Maoni katika picha
Siku kama ya leo mwezi mosi Safar mwaka (61h) ndio siku ambayo mateka wa nyumba ya Mtume Muhammad (s.a.w.w) waliwasili Sham, Majlisi anasema katika kitabu cha Biharu kutoka kwa Sahal bun Saadi Saaidiy kua: Nilitoka kwenda Baitul-Muqaddas nilipofika katikati ya Sham, nikaona mji wenye mito na miti mingi halafu kuna watu wanasherehekea wakiwa na wanawake wanaopiga dufu na ngoma, nikasema katika nafsi yangu, watu wa Sham hawana sikukuu ambayo mimi siifaham, nikaona watu wamekaa wanaongea, nikawaambia: Mimi ni Sahal bun Saadi nilimuona Muhammad (s.a.w.w). Wakasema: Ewe Sahal haikufurahishi kua mbingu hazinyeshi damu na ardhi haimezi waliojuu yake. Nikasema: kwa nini iwe hivyo? Wakasema: hiki ni kichwa cha Hussein mjukuu wa Muhammad (s.a.w.w) zawadi kutoka Iraq. Nikasema: Ajabu iliyoje! Kichwa cha Hussein kinatolewa zawadi na watu wanafurahi, nikasema: wataingia kwa mlango gani? Wakaonyesha mlango unao itwa: mlango wa saa. Akasema: wakati tukihojiana tukaona bendera zinafuatana, mara tukamuona mpanda farasi akiwa ameshika bendera huku kabeba kichwa ambacho uso wake ufanana zaidi na uso wa Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w), nyuma yake kukiwa na mwanamke aliyekaa juu ya ngamia isiyokua na kikalio, nikamsogelea na kumuuliza, wewe ni nani? Akasema: Mimi ni Sakina binti wa Hussein (a.s) nikamuuliza unashida yeyote? Mimi ni Sahal bun Saadi, nilimuona babu yako na kusikia hadithi zake, akasema: Ewe Sahal muambie huyu aliyebeba kichwa hiki atangulie mbele yetu ili watu wajishughulishe zaidi na kichwa hicho na wasiwaangalie maharim wa Mtume wa Mwenyezi Mungu. Sahal anasema: nikamfuata aliye beba kichwa nikamwambia, unaweza kunisaidia shida yangu na nitakupa dinari mia nne? Akasema: shida gani hiyo? Tanguliza kichwa mbele ya maharim, akafanya hivyo na mimi nikampa nilicho ahidi.

Sahal bun Saadi Saaidiy anasema: Nikamgeukia Ali bun Hussein (a.s) nikamuambia: Ewe kiongozi wangu unashida yeyote nikusaidie? Akasema: Unahela kidogo? Nikasema: Nina dinari elfu moja na noti elfu moja, akasema: chukua kidogo kalika hela zako umpe mbeba kichwa na umuambie atembee mbali na wanawake, Sahal akasema: nikafanya hivyo, kisha nikarudi kwake na kumuambia: ewe kiongozi wangu nimefanya kama ulivyo niambia, je kuna shida nyingine? Akasema: Ewe Sahal unanguo kuukuu? Nikasema: ewe kiongozi wangu unataka yanini, (mnakwenda kwa watu wanaovaa nguo za thamani wewe unaniomba nguo iliyo isha)? Akasema: Ewe Sahal nataka niiweke chini ya mnyororo hakika umeumiza shingo langu. Sahal anasema: Nikampa nguo, alipo inua mnyororo shingoni kwake damu zikachuruzika.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: