(Ra-asu Bishah) kituo cha mwanzo na mwisho wa Karbala pendwa.. picha za matembezi ya Arubaini (1441h)

Maoni katika picha
Sehemu: Ra-asu Bisha.

Muda: Mwezi mosi Safar (1441h).

Tukio: Kuanza matembezi ya Arubaini ya Imamu Hussein (a.s).

Ra-asu Bishah ni kisiwa kisicho kaliwa na watu, kipo kusini mwa mkoa wa Basra, umbali wa (km 100) kutoka katikati ya mji, sehemu hiyo huchukuliwa kua mwisho wa mpaka wa Iraq, baadhi ya waumini huanzia hapo matembeza ya ziara ya Arubaini ya Imamu Hussein (a.s) ambayo kilele chake ni mwezi (20) safar kila mwaka, hutumia kauli mbiu isemayo (Kutoka baharini hadi mtoni).

Umbali wa mahala hapo hadi Karbala kwenye malalo ya Imamu Hussei (a.s) ni kilometa (681) takriban, sehemu hiyo hushuhudia harakati maalum za kuanza misafara ya matembezi ya Arubaini inayo fanywa na mamilioni ya watu sambamba na majalisi za kuomboleza, makundi kwa makundi ya watu hushuka baharini kutawadha na kufanya ibada kisha huanza safari ya kwenda Karbala wakitokea mwishoni kabisha mwa mpaka wa Iraq upande wa kusini, hutembea wakiwa wamepandisha bendera na kusema (Labbaika yaa Hussein).

Mawakibu za kutoa huduma haziko mbali na sehemu hiyo, bali zipo hapohapo na zinaendelea kutoa huduma kwa kila zaairu huki wanasema kua mapinduzi ya Imamu Hussein (a.s) ni mpango wa Mwenyezi Mungu asiye shindwa, ni mshumaa uangazao, na kimbunga kiangushacho matwaghuti katika kila zama, na sharti lake ni kufuata mwenendo wake.

Kutokana na matembezi hayo watu wanaotoa huduma kwa mazuwaru wa Imamu Hussein (a.s) wameenea kila mahala, zamani matembezi yalikua yanaanzia katika msikiti wa Khatuwah wa Imamu Ali (a.s) uliopo katika wilaya ya Zubair magharibi ya Basra.

Kamera ya mtandao wa kimataifa Alkafeel kama kawaida yake kila mwaka ipo kila mahala na kwenye kila tukio kukuletea matembezi haya kuanzia mwanzo kabisa.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: