Miongoni mwa harakati za Quráni zinazo endelea kwa lengo la kuimarisha utamaduni wa Quráni, Maahadi ya Quráni tukufu tawi la Najafu chini ya Atabatu Abbasiyya, kwa mwaka wa pili mfululizo, inaandaa mihadhara ya Quráni kuhusu Imamu Hussein (a.s), na kuwaalika wasomi wa hauza pamoja na waumini, wametoa mada mbalimbali kuhusu Imamu Hussein (a.s) na kuowanisha na changamoto za jamii ya sasa, sambamba na kuzitafutia ufumbuzi kwa mujibu wa mwenendo wa Ahlulbait (a.s).
Program hiyo imefunguliwa kwa Quráni tukufu, kisha ukatolewa mhadhara wa kwanza na Sayyid Muhammad Swadiq Khurasani uliokua unasema: (Pamoja na Imamu Hussein –a.s- katika vituo vya kibinadamu), alielezea changamoto nyingi za kijamii pamoja na njia za utatuzi wake, aidha ameeleza baadhi ya mitazamo mibaya ya watu, na kutoa ushahidi kutoka kwenye turathi za maimamu wetu (a.s) hadithi na riwaya.
Kumbuka kua ratiba hii ya mihadhara hufanywa kila mwaka na hualikwa wasomi wa hauza kutoka Najafu Ashrafu.