Kutokana na wingi wa huduma zinazo tolewa na mgahawa wa Atabatu Abbasiyya kwenye kipindi cha ziara ya Arubaini, na kwa ajili ya kutoa huduma bora kwa mazuwaru wengi zaidi, mwaka huu wanatarajiwa kuwa wengi zaidi ya mwaka jana, aidha kutokana na wingi wa madirisha ya kugawa chakula kwa mazuwaru katika vituo vya nje na vya ndani, kama vile mgahawa wa Ataba wa nje kwenye jengo la Alqami, Kuleini na mengine, au ndani ya Ataba na maeneo yanayo izunguka.
Kitengo cha mgahawa (mudhifu) kimetangaza kua kimejipanga kununua mikate na mifugo (wanyama) kutoka kwa wananchi wa Iraq, kwa ajili ya kuhakikisha wanapata nyama nyingi zitakazo endana na idani ya mazuwaru wanao tarajiwa kuingia Karbala tukufu, kwa maelezo zaidi wasiliana nasi kwa namba za simu zifuatazo (07801371180 au 07700284921).