Idara ya mahusiano ya vyuo vikuu yaanza maandalizi ya kushiriki katika mkakati wa ziara ya Arubaini kwa kuwasaidia waliopotelewa na kupotezana

Maoni katika picha
Idara ya mahusiano ya vyuo vikuu chini ya kitengo cha mahusiano cha Atabatu Abbasiyya tukufu imeanza maandalizi maalum ya ziara ya Arubaini katika sekta ya waliopotelewa na walio kupotezana, kwa kufanya kikao maalum na viongozi wa vituo vya kushughulikia walio potelewa kwenye ziara ya Arubaini, pamoja na watu wa idara ya mawasiliano katika kitengo cha miradi ya kihandisi na shirika la Nurul-Kafeel na wawakilishi wa wizara ya mafuta na wizara ya mambo ya ndani pamoja na baadhi ya wanafunzi wakujitolea.

Kiongozi wa idara Ustadh Azhar Rikabi ameuambia mtandao wa Alkafeel kua: “Sisi katika idara ya mahusiano ya vyuo vikuu tulitangaza utayari wetu kama tunavyo fanya kila mwaka, tunatoa idadi kubwa ya watumishi wa kujitolea na kuwasambaza katika vituo vya waliopotelewa na kupotezana, vilivyopo katika barabara zinazo elekea Karbala sambamba na kwenye vituo vilivyopo ndani ya Karbala”.

Akaongeza kua: “Hakika watumishi wa kujitolea wana ujuzi na uzowefu katika sekta hiyo, wanatoka kwenye vyuo vikuu na Maahadi za hapa Iraq, huteuliwa na muwakilishi wa idara kutoka vyuo vikuu tofauti vya Iraq”.

Kumbuka kua swala hili linafanyika kufuatia msongamano mkubwa wa mazuwaru katika mji wa Karbala na barabara zinazo elekea kwenye mji huo, mamilioni ya watu hutembea kwa miguu kuja kwenye ziara tukufu, ziara ya Arubaini ya Imamu Hussein (a.s), kila mwaka Atabatu Abbasiyya hujenga mabanda maalum kwa ajili ya kushughulikia walio potelewa au walio potezana sehemu zote za barabara, kwa ajili ya kusaidia kuwakutanisha walio potezana miongoni mwa watoto, wazee na wengine.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: