Msafara wa misaada ya kibinadamu Alwafaa chini ya kikosi cha Abbasi (a.s) cha wapiganaji (Liwaa/26 Hashdi Shaábi) kutoka mji mkuu wa Bagdad umeelekea katika mkoa wa Muthanna kusaidia watoto wa mashahidi na masikini, kufuatia kuanza mwaka mpya wa masomo, wakiwa na tani nne za misaada.
Tumeongea na mkuu wa msafara huo bwana Fadhili Hamdani amesema kua: “Hakika msafara huu ni sehemu ya kufanyia kazi aya tukufu za Quráni na hadithi za Ahlulbait (a.s) zinazo himiza elimu na kusaidia watu, tumekuja na vitu vitakavyo wafaa katika mwaka mpya wa masomo, miongoni mwa vitu hivyo ni nguo, vifaa vya shule, vifaa vya umeme na vinginevyo”.
Muwakilishi wa kikosi cha Abbasi katika mkoa wa Muthanna Ustadh Saadi Abdaliy amesema kua: “Kwa kushirikiana na msafara wa misaada ya kibinadamu Alwafaa na ofisi ya biashara ya mkoa, watoto wote wa mashahidi wa Hashdi Shaábi pamoja na mayatima wengine na masikini watapewa misaada, chini ya maelekezo ya Marjaa Dini mkuu na Atabatu Abbasiyya pamoja na uongozi wa kikosi cha Abbasi na kamati ya kusaidia familia za mashahidi na masikini”.
Familia za mashahidi zimeshukuru msaada huu wa kibinadamu kwa familia za mashahidi na masikini kwani unasaidia kupunguza shida zao, kwa kuwapatia mahitaji muhimu ya shule katika mwaka mpya wa masomo.