Balozi wa Pakistani nchini Iraq Ustadh Saajid Bilali amefurahishwa na makumbusho ya Alkafeel, kutokana na vifaa kale vilivyopo ndani ya makumbusho hiyo ambavyo ni vya miongo tofauti, aidha amepongeza mpangilio wa vifaa hivyo ndani ya Maktaba.
Yametokea hayo kwenye ziara iliyo fanywa na balozi huyo katika Atabatu Abbasiyya tukufu na kutembelea makumbusho ya Alkafeel ya vifaa na nakala kale, katika matembezi hayo alifuatana na jopo la viongozi wa Atabatu Abbasiyya pamoja na wasimamizi wa makumbusho, akapewa maelezo ya kina kuhusu vitu vilivyomo ndani ya makumbusho hiyo pamoja na baadhi ya nakala kale adimu, sehemu nyingi alikua anasimama kwa muda mrefu kuangalia vifaa kale.
Mwishoni mwa ziara Mheshimiwa balozi wa Pakistani ameonyesha furaha yake kwa musema: “Nifuraha kubwa kwangu kutembelea malalo ya Abulfadhil Abbasi (a.s) katika mwezi wa Muharam, na kuonyesha heshima yangu kwa watu wa nyumba ya Mtume (a.s) na wafuasi wao”.
Akaongeza kua: “Nimeridhishwa na mapokezi mazuri ya viongozi wa Atabatu Abbasiyya tukufu, nawatakia mafanikio mema kwa huduma wanazo toa kwa jamii”.