Marjaa Dini mkuu ashauri namna ya kutatua matatizo ya kitaifa na kutekeleza maombi ya wananchi, aidha ameikumusha serikali ushauri wa kumaliza matatizo ya raia aliotoa mwaka 2015m

Maoni katika picha
Marjaa Dini mkuu ametoa ushauri kuhusu matukio yanayo shuhudiwa hapa Iraq siku hizi, na amekumbusha ushauri kama huo aliotoa mwaka 2015m kuhusu kutatua matatizo ya kitaifa na kumaliza changamoto za raia, ameyasema hayo katika khutuba ya pili ya swala ya Ijumaa leo (5 Safar 1441h) sawa na (4 Oktoba 2019m), iliyo swaliwa ndani ya ukumbi wa haram ya Imamu Hussein (a.s) chini ya uimamu wa Mheshimiwa Sayyid Ahmadi Swafi, ifuatayo ni nakala ya khutuba hiyo:

Enyi mabwana na mabibi:

(Nakusomeeni ujumbe uliotufikia kutoka ofisi ya Mheshimiwa Marjaa Dini mkuu katika mji wa Najafu).

Katika siku za hivi karibuni yamefanyika mambo yasiyo kubalika kwa watu wanaofanya maandamano ya amani, na uharibifu wa mali za umma na binafsi katika mji wa Bagdad na kwenye mikoa mingine, maandamano hayo yamesababisha uharibifu mkubwa ikiwa ni pamoja na kumwagika damu na watu wengi wamejeruhiwa, sambamba na kufanywa uharibifu mkubwa katika taasisi za serikali na za umma, jambo la kusikitisha zaidi ni pale matukio haya yanapo fanana na yaliyo tokea miaka ya nyuma.

Marjaa Dini mkuu kila anapo shauri wenye madaraka serikalini wabadilishe mwenendo wao katika kushughulikia matatizo ya taifa, na kufanya jitihada za kweli za kurekebisha mambo na kupambana na ufisadi pamoja na kurekebisha utendaji katika idara za serikali, na kuwatahadharisha wanaozuwia marekebisho na kupuuza matakwa ya raia na kuwataka watambue kua kurekebisha mambo ni lazima hakuna pa kukwepea, hata kama sauti za kudai haki zikipungua wajue kua zitarudi wakati mwingise kwa nguvu zaidi ya mara ya kwanza. Leo Marjaa anasisitiza kwa mara nyingine mambo aliyo yasema toka zamani, anatoa wito kwa mihimili ya serikali ichukue hatua za vitendo katika kurekebisha mambo, anautaka mhimili wa benge uchukue nafasi yake kisheria katika kutafuta ufumbuzi wa tatuzo hili, bunge liisimamie serikali kurekibisha mambo yanayo takiwa kurekebishwa na yaonekane wazi.

Hali kadhalika mhimili wa mahakama na vyombo vya usalama wanajukumu kubwa la kupambana na ufisadi na kuhakikisha mali zilizo ibwa na mafisadi zinarudi kwa raia, bahati mbaya mhimili huu hauja tekeleza majukumu yake ipasavyo katika siku za nyuma, hali ikiendelea kua hivyo itakua hakuna faida ya kua na sheria ya kupambana na ufisadi hapa nchini.

Serikali inatakiwa kuamka na kutekeleza wajibu wake, ihakikishe inafanyia kazi changamoto za wananchi, kwa kuboresha huduma za msingi na kuongeza nafasi za ajira bila upendeleo pamoja na kukamilisha mafaili ya watu waliochezea mali za umma na kuwafikisha mahakamani.

Fahamu kau ofisi ya Marjaa iliwahi kuzungumza mambo haya tarehe saba Agosti mwaka 2015m wakati wananchi walipo fanya maandamano ya kudai marekebisho, alisema kau: (Iundwe kamati ya wataalam maarufu walio nje ya serikali, wenye ujuzi mkubwa na wasiokua na tuhuma zozote, kamati hiyo ipewe jukumu la kuandaa mpango mkakati wa kupambana na ufisadi na kutekeleza madai ya wananchi, wajumbe wa kamati hiyo wapewe uwezo wa kuchunguza kwa kina idara zote za serikali, pia wawakilishi wa waandamanaji kutoka kila mkoa wapewe nafasi ya kuongea mahitaji yao, baada ya kamati hiyo kukamilisha mpango mkakati huo utakao baini changamoto na namna ya kuzitatua kisheria na kiutendaji, utahitaji ufanyiwe kazi hata kwa kusaidiwa na Marjaiyya pamoja na wananchi).

Mapendekezo haya hayakufanyiwa kazi, iwapo yakifanyiwa kazi hivi sasa inaweza kua njia nzuri ya kumaliza tatizo lililopo.

Nimatumaini yetu viongozi watatanguliza maslahi ya taifa na kuwahi kurekebisha mambo kabla hayajaharibika zaidi, tunatarajia wajiepushe na kutumia nguvu dhidi ya waandamanaji.

Tunamuomba Mwenyezi Mungu mtukufu aijaalie kila la kheri Iraq na raia wake.

Amani ya Mwenyezi Mungu iwe juu yenu na baraka zake na rehema zake.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: