Kwa utaalamu wa hali ya juu: kituo cha uzalishaji wa vipindi Alkafeel kimetengeneza masafa ya bure inayo tumika kurusha matukio ya matembezi ya Arubaini

Maoni katika picha
Kituo cha uzalishaji wa vipindi Alkafeel chini ya kitengo cha habari na utamaduni kimetengeneza masafa yenye ubora wa hali ya juu, kwa ajili ya kurusha matembezi ya wapenzi wa Imamu Hussein (a.s) bure tena kwa muonekano bora kabisa (clean), kuanzia kituo cha mbali kusini mwa Iraq hadi katika kilele cha ushujaa na msimamo Karbala tukufu, kwa kutumia mitambo ya kisasa zaidi inayo endeshwa na watu walio bobea katika fani hiyo, wanafanya kila wawezalo kufikisha sauti ya ziara hii na matukio yake kila kona ya dunia.

Kituo kimetoa wito kwa vyombo vyote vya habari vya kitaifa na kimataifa vinavyo penda kurusha matukio hayo vitumie anuani zifuatazo:

E3B at 3°E
Down:11578.9 H
SR:2400
Mod: DVBS28PSK
FEC:5/6
HD/MPEH-4
matangazo yanafanyika kila siku kuanzia saa (2:00 asubuhi) hadi saa (4:30 asubuhi), halafu wanaelekea ndani ya Atabatu Abbasiyya tukufu kurusha matukio ya swala ya Adhuhuri na Alasiri, kisha wanarudia kurusha matembezi kuanzia saa (9:30 jioni) hadi saa (11:45 jioni), halafu wanahamia kwenye kutangaza matukio ya swala ya Magharibi na Isha.

Kwa maelezo zaidi unaweza kuwasiliana na muhandisi wa matangazo haya kwa namba (+9647814164773) kwa wale wanaotumia mitandao tumeandaa ukurasa maalum wa facebook kupitia anuani ifuatayo:

https://m.facebook.com/alkafeel.for.artistic.production/
na kwenye yutube kwa anuani ifuatayo:

https://www.youtube.com/channel/UCaaBs5EwkPCs1wXIeMPP0b
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: