Watumishi wa Ataba mbili tukufu watoa pole kwa Imamu Hussein na ndugu yake Abulfadhil Abbasi (a.s) katika kuomboleza kifo cha ndugu yao Imamu Hassan (a.s)

Maoni katika picha
Watumishi wa Ataba mbili tukufu Husseiniyya na Abbasiyya wanaomboleza kifo cha mjukuu wa Mtume Muhammad (s.a.w.w) Hassan Azzakii Almujtaba (a.s) kilicho tokea mwezi saba Safar, kwa kufanya matembezi (maukibu) ya uombolezaji ya pamoja, iliyo jumuisha viongozi na watumishi wa Atabatu Abbasiyya, wakiongozwa na katibu mkuu Mhandisi Muhammad Ashiqar kwa ajili ya kutoa pole kwa Imamu Hussein na Abulfadhil Abbasi (a.s) kufuatia msiba huu.

Baada ya kutoa pole kwa Abulfadhil Abbasi (a.s) ndani ya ukumbi wa haram yake tukufu mfasara (maukibu) ikaelekea kwenye malalo ya Abu Abdillahi Hussein (a.s) huku wamebeba jeneza la kuigiza la Imamu Almujtaba (a.s), wakapita katika uwanja mtukufu wa katikati ya haram mbili, na wakapokelewa na watumishi wa Atabatu Husseiniyya tukufu halafu wakafanya majlis ya kuomboleza ndani ya haram ya Imamu Hussein (a.s) sambamba na kusomwa kaswida na tenzi za kuomboleza zilizo eleza dhulma aliyo fanyiwa Imamu huyu na yaliyo jiri dhidi yake, aidha ndani ya ukumbi wa utawala katika Atabatu Abbasiyya imefanyika majlis ya kuomboleza kwa watumishi wake.

Fahamu kua Ataba tukufu za Karbala hufanya matembezi maalum ya kuomboleza katika tarehe za vifo vya watu wa nyumba ya Mtume (a.s) katika kipindi cha mwaka mzima.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: