Atabatu Abbasiyya tukufu imekamilisha ujengaji wa vituo vya kuelekeza walio potelewa na kupotezana na imesema kua kuna ongezeko la vituo na aina ya huduma zake

Maoni katika picha
Idara ya mawasiliano katika Atabatu Abbasiyya tukufu chini ya kitengo cha miradi, imetangaza kukamilika kwa kazi ya kujenga vituo vinavyo shughulikia walio potelewa au kupotezana, kwa ajili ya kulinda watoto na wazee wasipotee, pia kuhakikisha wanapatikana kwa urahisi iwapo watapotezana na wasimamizi wao kutokana na msongamano mkubwa wa mazuwaru wa Arubaini.

Kwa mujibu wa maelezo ya Mhandisi Farasi Hamza kiongozi wa idara hiyo, amesema kua: Ufunguzi wa vituo hivi unatokana na umuhimu wa kushughulikia walio potelewa au walio potezana katika ziara ya Arubaini ya Imam Hussein (a.s), pia program hii imekua na matokeo mazuri katika ziara zilizo pita.

Akaendelea kusema kua: “Katika kuendeleza huduma hii, kutokana na matarajio ya kuongezeka kwa idadi ya mazuwaru mwaka huu tofauti na miaka ya nyuma tumeongeza idadi ya vituo pamoja na huduma zinazo tolewa, tumeongeza zaidi ya vituo (18) huku vituo (15) vikiwa upande wa mji wa Musayyib, ambavyo vimefunguliwa kwa kushirikiana na askari wa ulinzi, na zaidi ya vituo vitatu vipo katika mkoa wa Diwaniyya, kutokana na mkoa huo kua na msongamano mkubwa wa mazuwaru, mwaka huu tumetengeneza mtandao maalum wa mawasiliano yetu, vituo vyote vimewekewa mawasiliano hayo salama zaidi kati yetu”.

Akabainisha kua: “Vituo hivyo vinaendeshwa na watalamu miongoni mwa wanafunzi wa vyuo vikuu na Maahadi za Iraq, walio patikana kupitia idara ya mahusiano ya vyuo vikuu katika Atabatu Abbasiyya na wanafanya kazi kwa kujitolea baada ya kuwapa semina maalum na kufanya mikutano mbalimbali vya kuwabainishia majukumu na wajibu wao”.

Kumbuka kua vituo vya kushughulikia walio potelewa au kupotezana ni sehemu ya huduma zinazo tolewa na Atabatu Abbasiyya tukufu kwa mazuwaru, katika ziara iliyo pita vilifanikiwa kuwakutanisha maelfu ya mazuwaru walio potezana, fahamu kua vituo hivi vina program ya kielektronik yenye ukurasa wa maelezo uliounganishwa kwenye vituo vyote, kituo kimoja kinapo andika taarifa za mtu aliye potea au kupotelewa, taarifa hiyo huonekana moja kwa moja katika vituo vyote.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: