Kukamilika kwa kazi ya kutengeneza daraja maalum la chuma litakalo tumiwa na mazuwaru wa Arubaini na mawakibu za kuomboleza kwa muda

Maoni katika picha
Miongoni mwa maandalizi maalum ya ziara ya Arubaini ya Imamu Hussein (a.s), mafundi wa kitengo cha usimamizi wa kihandisi katika Atabatu Abbasiyya tukufu wamekamilisha kazi ya kufunga daraja la chuma litakalo tumiwa na mazuwaru wa Arubaini ya Imamu Hussein (a.s).

Daraja hilo hufungwa kila mwaka kwa ajili ya kurahisisha upitaji wa mazuwaru wakati wa ziara na kuondoa mgongano baina yao na mawakibu Husseiniyya kutoka ndani na nje ya taifa.

Lipo upande wa kusini magharibi ya Atabatu Abbasiyya tukufu mbele ya mlango wa Imamu Hassan (a.s), kitengo cha usimamizi wa kihandisi katika Atabatu Abbasiyya hufunga daraja hilo kila mwaka, na madaraja mengine mawili hufungwa na kitengo cha uangalizi katika Atabatu Husseiniyya, kwa ajili ya kupunguza msongamano wakati wa ziara pamoja na kuondoa mgongano wa mazuwaru na mawakibu za kuomboleza.

Madaraja hayo yanaundwa kwa vyuma ambavyo huonganishwa na kufungwa kihandisi, yana upana wa (mita 8) na yamegawanyika sehemu mbili, kila sehemu inaupana wa (mita 4), urefu wake wa kwenda juu ni zaidi ya (mita 4), halafu kuna vipande vya mbao kila kimoja kina urefu wa (mita 2.40) na upana wa (mita 1.22), mbao hizo zimewekwa pembezoni mwa daraja kwa ajili ya kuimarisha usalama kwa mazuwaru wakati wakipita.

Kumbuka kua Atabatu Abbasiyya tukufu kupitia vitengo vyake vyote, kikiwemo kitengo cha uangalizi wa kihandisi, imetangaza kukamilika kwa maandalizi ya lazima kwa ajili ya kuwapokea mazuwaru wa ziara ya Arubaini ya Imamu Hussein (a.s).
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: