Kituo cha upigaji picha nakala kale na faharasi chakamilisha upigai picha (562) wa nakala kale katika maktaba ya Shekh Ibrahim Al-Aamili Albayadhi

Maoni katika picha
Katika utaratibu wa kushirikiana baina ya Atabatu Abbasiyya kupitia kituo cha upigaji picha nakala kale na faharasi chini ya maktaba na taasisi za turathi zinazo hudumia watafiti na wahakiki, kwa kuwaandalia nakala chini ya utaratibu endelevu, wamepiga picha nakala kale za maktaba ya Shekh Ibrahim bun Ali bun Suleiman Al-Aamili Albayadhi katika mkoa wa Junuub (wilaya ya Suwaru) nchini Lebanon, jumla ya nakala kale zilizo pigwa picha ni (562), zinazo elezea elimu tufauti, chini ya watalam wa kituo cha upigaji picha nakala kale na faharasi”. Maktaba ya Shekh Ibrahim Albayadhi (r.a) ni miongoni mwa maktaba binafsi kubwa inayo tembelewa na watu wengi wanaofanya tafiti na uhakiki, kwani inahazina kubwa ya nakala kale, Shekh Ibrahim bun Ali bun Suleiman Al-Aamili Albayadhi alifariki mwaka (1424h) alikua mwanachuoni mkubwa, mwaka (1926m) alisafiri kwenda Nafafu kusoma elimu ya Dini, kisha akarudi Jabal-Aamir mwaka (1930m), akakaa miaka miwili anafanya kazi za kijamii na kufundisha halafu akarudi Najafu mwaka (1932) kuendelea na masomo, akarudi tena Jabal-Aamir mwaka (1940m) akaishi katika mji wa (Albayaadh) hadi mwaka (1961m) akaenda Kuwait kwa ombi la Marjaa Dini mkuu wakati huo Ayatullahi Sayyid Muhsin Alhakiim, akawa Qadhi wa madh-habu ya Jaafariyya katika nchi hiyo kwa muda wa miaka kumi, kuanzia mwaka (1961m).

Fahamu kua kituo cha kupiga picha nakala kale na faharasi chini ya idara ya maktaba ya Atabatu Abbasiyya tukufu, kinajukumu la kupiga picha nakala kale na kuzitengenezea faharasi kwa ajili ya kumrahisishia mtu anaye fanya tafiti na uhakiki, kituo hicho kimesha kiga picha nakala kale nyingi za kiarabu na kiislamu katika miji tofauti ya Iraq na ulimwengu wa kiislamu.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: