Kikosi cha Abbasi (a.s) cha wapiganaji kimekutana na viongozi wa kikosi cha Furaat Ausat na wamejadili kuhusu kuimarisha ulinzi katika ziara ya Arubaini

Maoni katika picha
Miongoni mwa maandalizi ya kuimarisha usalama katika ziara ya Arubaini, vingozi wa kikosi cha Abbasi (a.s) cha wapiganaji (Liwaa/26 Hashdi Shaábi) na viongozi wa kikosi cha Furaat Ausat wamefanya kikao na kupanga majukumu ya kuimarisha ulinzi na usalama kwenye ziara ya Arubaini inayo hudhuriwa na mamilioni ya watu.

Kiongozi mkuu wa kikosi cha Abbasi Ustadh Maitham Zaidi amesema kua: “Kikosi kulitoa tahadhari ya kuimarisha usalama ulipo karibia msimu wa ziara inayo hudhuriwa na mamilioni ya watu, sambamba na matukio yanayo shuhudiwa katika taifa hili, adui asije akatumia mazingira haya kuwashambulia mazuwaru”, akabainisha kua: “Vikosi vya Abbasi vimejipanga kuanzia kaskazini magharibi ya Karbala hadi mji wa Nukhaibu, kwa kipindi cha miaka minne sasa kikosi hiki kimekua kikisimamia ulinzi wa jangwa kubwa zaidi linalo zingatiwa kua ni theluthi ya Iraq, kwani jangwa hilo linafika hadi Ramadi na kwenye viunga vya Najafu”, akasema kua wameongeza wapiganaji wa hakiba.

Kiongozi wa kikosi cha Furaat Ausat Qaiss Khalfu Rahima amesema kua: “Kikao cha leo pamoja na viongozi wa kikosi chenye jukumu kubwa ni muhimu sana, kwani kikosi cha Abbasi kinaimarisha usalama kwenye eneo kubwa na kimeongeza zaidi ya wapiganaji elfu (5) ambao wamekua wakijitolea kila mwaka, wanasaidia katika ukaguzi na kupangilia matembezi ya mazuwaru”.

Akasema: “Kikao cha leo kilijikita katika kuainisha majukumu ya vikosi vya wapiganaji na wale wanao jitolea kupitia kitengo cha Abbasi”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: