Mtandao wa kimataifa Alkafeel unatoa wito kwa wafuasi wa Ahlulbait (a.s) duniani kote, wale ambao wameshindwa kuja katika ardhi ya Twafu kufanya ziara ya Arubaini ya bwana wa vijana wa peponi na ndugu yake, watoto wake na wafuasi wake wema (a.s) wasajili majina yao katika ukurasa wa ziara kwa niaba.
Kama sehemu ya kufanyia kazi kauli ya Imamu Muhammad Hassan Askariy (a.s) isemayo: (Alama za muumini ni tano: kuswali rakaa hamsini na moja, kufanya ziara ya Arubaini, kuvaa pete mkono wa kulia, kugusa paji la uso chini, kusoma kwa sauti bismilaahi rahmaani rahiim) mtandao umeandaa watumishi watakao fanya ziara ya Imamu Hussein na ndugu yake Abulfadhil Abbasi (a.s) na kusoma dua kwa niaba ya kila atakaesajili jina lake katika ukurasa wa ziara kwa niaba.
Kumbuka kua idadi ya watu waliojisajili mwaka jana na wakafanyiwa ziara ilikua zaidi ya watu laki moja (100,000) kutoka kila kona ya dunia, miongoni mwa walio fanya ziara kwa niaba ni muwakilishi wa Marjaa Dini mkuu Mheshimiwa Sayyid Ahmadi Swafi na katibu mkuu wa Atabatu Abbasiyya tukufu pamoja na jopo la wanachuoni watukufu wageni wa Atabatu Abbasiyya tukufu.