Sayyid Sistani awahusia mazuwaru wa Imamu Hussein (a.s): Allah Allah katika swala

Maoni katika picha
Miongoni mwa usia na maelekezo yaliyo tolewa na ofisi ya Marjaa Dini mkuu Ayatullah Sayyid Sistani kwa mazuwaru wa ziara ya Arubaini ya Imamu Hussein (a.s), alio sisitiza na kuupa kipao mbele zaidi ni swala, inatakiwa iswaliwe kwa wakati, ukizingatia kua ni miongoni mwa vitendo vinavyo pendeza zaidi mbele ya Mwenyezi Mungu mtukufu, kumzuru Hussein (a.s) ni mustahabu lakini swala ni wajibu, swala ndio inayo kukurubisha kwa Mwenyezi Mungu kupitia Imamu Hussein (a.s), ameyasema hayo alipokua akijibu swali kutoka kwa waumini walio omba nasaha zake, katika mtandao wake maalum yameandikwa maneno yafuatayo:

Allah Allah katika swala hakika –kama ilivyo kuja katika hadithi tukufu- ni nguzo ya Dini na ngazi ya Muumini, ikikubaliwa na ibada zingine zitakubaliwa na ikikataliwa na ibada zingine zitakataliwa, inatakiwa kuswaliwa mwanzoni mwa wakati wake, hakika ni ibada inayo pendwa zaidi na Mwenyezi Mungu, humjibu haraka anaye muomba akiwa katika ibada hiyo, muumini hatakiwi kushughulika na jambo lingine wakati wa swala unapo ingia, hakika swala ndio ibada bora zaidi, imepokewa kutoka kwa Maimamu (a.s) kauli isemayo: (Hatapata shifaa yetu mwenye kupuuza swala). Imepokewa kutoka kwa Imamu Hussein (a.s) namna alivyo swali katika mazingira magumu siku ya Ashura, alimuambia yule aliye mkumbushwa swala mwanzoni mwa wakati wake: (umekumbuka swala, Mwenyezi Mungu akujaalie katika wenye kuswali na wakumbukao) akaswali katika uwanja wa vita huku anashambuliwa mishale.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: