Muhimu… nakala kamili ya khutuba ya Ijumaa: Marjaa Dini mkuu amesisitiza kua haegemei upande wowote ispokua upande wa raia na hatetei ispokua maslahi yao

Maoni katika picha
Marjaa Dini mkuu amesisitiza kua haegemei upande wowote ispokua upande wa raia wala hatetei ispokua maslahi yao, hana maslahi au uhusiano na upande wowote wa watawala, asisitiza aliyo sema Aprili mwaka (2006m) wakati wa kuunda serikali karibu na uchaguzi mpya wa mara ya kwanza wa bunge kua: (Hata mfumbia macho yeyote atakaye haribu maslahi ya raia wa Iraq, ataangalia utendaji wa serikali na kuonyesha kila sehemu yenye kasoro pale itakapo lazimika, sauti yake daima itakua pamoja na sauti za wadhulumiwa katika taifa hili popote watakapo kua bila kutofautisha milengo yao na tabaka zao).

Ameyasema hayo katika khutuba ya pili ya swala ya Ijumaa leo (12 Safar 1441h) sawa na (11 Oktoba 2019m) iliyo swaliwa ndani ya ukumbi wa haram ya Imamu Hussein (a.s), chini ya uimamu wa Mheshimiwa Shekh Abdulmahdi Karbalai, ifuatayo ni nakala ya khutuba hiyo:

Mabwana na mabibi tunakusomeeni nakala iliyo tufikia kutoka ofisi ya Mheshimiwa Marjaa Dini mkuu katika mji wa Najafu: katika khutuba ya Ijumaa iliyo pita alikemea na kulaani vitendo wanavyo fanyiwa waandamanaji na wanajeshi, kwenye maadamano yaliyo shuhudiwa wiki iliyo pita, pia alilaani vitendo vya kuchoma moto na kuharibu mali za serikali na binafsi katika maandamano hayo. Akazitaka pande zote zijizuwie kutumia nguvu katika maandamano hayo.

Lakini tukashuhudia kuongezeka kwa utumiaji wa nguvu kwa waandamanaji, na unyanyasaji wa wazi kwa baadhi ya vyombo vya habari na kuwazuwia wasiripoti kinacho endelea katika uwanja wa waandamanaji.

Wakati ambao imetangazwa kua imetolewa amri kwa wanajeshi wasitumie risasi kwa waandamanaji, wameshambuliwa maelfu ya waandamanaji baadhi yao wamefariki na wengine wengi wamejeruhiwa katika mji wa Bagdad, Naswiriyya, Diwaniyya na miji mingine, kwa kufyatuliwa risasi moja kwa moja, wamefanyiwa ukatili wa hali ya juu.

Serikali na vyombo vya ulinzi na usalama wanawajibika kwa damu ya waandamanaji iliyo mwagika, sawa iwe damu ya waandamanaji au askari. Serikali inawajibika pale baadhi ya askari wake wanapo tumia nguvu kubwa dhidi ya waandamanaji, hata kama hawajafuata maelekezo waliyo pewa, au hawajafundishwa namna ya kuamiliana na vurugu za wananchi bila kutumia nguvu kipita kiasi.

Inawajibika pale askari wake watakapokua hawafuati utaratibu kwa kuwashambulia waandamanaji na waandishi wa habari kwa kutaka kuwahofisha.

Inawajibika pale askati wake watakapo shindwa kulinda raia na mali zao pamoja na taasisi za serikali na binafsi dhidi ya idadi ndogo ya maharamia wanaojichomeka ndani ya waandamanaji, kwa lengo la kuondoa amani kwa waandamanaji.

Hakika Marjaa Dini mkuu analaani vikali umwagaji damu uliofanywa, na anawapa pole wafiwa wote pamoja na majeruhi, anaungana na madai ya wale wanao fanya maandamano ya amani, anaitaka serikali ifanye uchunguzi wa haraka na kubaini kila aliyevunja sheria katika kuamiliana na waandamanaji, na kuwekwa wazi taarifa ya uchunguzi huo, watu wote watakao kutwa na hatia wafikishwe katika vyombo vya sharia bila kuangalia nafasi zao na milengo yao, jambo hilo lifanyike ndani ya muda maalumu –wiki mbili kwa mfano- wala yasitokee kama yaliyo tokea siku za nyuma.

Hakika mambo haya yana umuhimu mkubwa kwa sasa, yataonyesha ukweli wa serikali katika kushughulikia madai ya waandamanaji, sio rahisi kufanya marekebisho yeyote bila serikali kuonyesha kua inafuata utawala wa kisheria na kutovunja katiba, na kuwaadhibu wanaovunja sheria. Marjaa Dini mkuu hana maslahi wala uhusiano binafsi na mlengo wowote wa watawala, wala haegemei upande wowote tofauti na upande wa raia na wala hatetei ispokua maslahi yao, anasisitiza aliyo sema Aprili mwaka (2006m) wakati wa kuunda serikali baada ya uchaguzi wa kwanza wa bunge, alisema kua: (Hata mfumbia macho yeyote atakaye haribu maslahi ya raia wa Iraq, ataangalia utendaji wa serikali na kuonyesha kila sehemu yenye kasoro pale itakapo lazimika, sauti yake daima itakua pamoja na sauti za wadhulumiwa katika taifa hili popote watakapo kua bila kutofautisha milengo yao na tabaka zao).

Hakuna hila wala nguvu ispokua ni za Mwenyezi Mungu mkuu.

Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: