Hii ndio picha ya mapinduzi ya mapenzi na utiifu kwa Imamu Hussein unaofanywa na wapenzi na wafuasi wake katika kila zama, bado misafara ya mazuwaru wa Imamu Hussein (a.s) inaendelea kumiminika katika mkoa wa Dhiqaar, Muthanna na Diwaniyya wakija kumzuru Imamu (a.s) katika kumbukumbu ya Arubaini yake tukufu, na kutangaza utiifu wao kwake kwa namna isiyo weza kuelezeka.
Mawakibu za kutoa huduma zimejaa njia zote zinazo tumiwa na mazuwaru, zinatoa huduma za aina mbalimbali, wanajitolea kwa hali na mali, pamoja na kuwepo kwa vituo vya afya, askari wameenea kila kona kuimarisha usalama wa mazuwaru, kamera ya Alkafeel inakuletea picha za matembezi hayo kutoka kwenye moja ya barabara zinazo elekea Karbala.