Miji ya katikati na kusini mwa Iraq inashuhudia mamilioni ya mazuwaru wanaokwenda katika malalo ya Imamu Hussein (a.s), kufanya ziara ya Arubaini, misafara ya watu wanaokwenda kwa miguu imewasili katika mikoa ya kusini maeneo ya mkoa wa Muthanna, sehemu ya mpakani na mkoa wa Qadisiyya ambao njia zake zote zimejaa watu wanao toa huduma kwa mazuwaru.
Barabara za mji huo zimejaa mazuwaru, upo umbali wa kilometa (300) kutoka Karbala, wamebakiza siku saba tu kufika kilele cha ziara ya Arubaini (20 Safar), watu wa mji huu ni wakarimu sana, wanatoa mapokezi mazuri na huduma bora zaidi kwa mazuwaru.
Kamera ya mtandao wa kimataifa Alkafeel inakuletea picha za mazuwaru na huduma wanazo pewa katika miji hiyo.