Kutokana na msongamano mkubwa: umetengenezwa uzio unaotenganisha mazuwaru wanao kwenda sehemu ya Maqaam ya mkono mtukufu wa Abulfadhil Abbasi (a.s)

Maoni katika picha
Kitengo cha uangalizi wa kihandisi katika Atabatu Abbasiyya tukufu ikiwa kama sehemu ya majukumu yake kwenye ziara ya Arubaini ya Imamu Hussein (a.s), kimetengeneza uzio wa mbao katika Maqaam ya mkono wa Abulfadhil Abbasi (a.s) iliyopo mkabala na mlango wa Imamu Ali (a.s), sehemu hiyo huwa na msongamano kubwa unao tatiza matembezi ya mazuwaru.

Uzio umetenganisha upande wa wanaume na wanawake na kurahisisha upitaji wa mazuwaru sehemu hiyo.

Baada ya kuwekwa mazuwaru uzio huo, mazuwaru wamekua wakipita kwa urahisi bila kusababisha msongamano.

Kumbuka kua mafundi wanao fanya kazi katika kitengo cha usimamizi wa kihandisi walianza mapema kufanya maandalizi ya kuwapokea mazuwaru wa Arubaini, mwaka huu unatarajiwa kuwa na idadi kubwa zaidi ya mazuwaru, kwa ajili ya kuhakikisha wanapewa huduma bora kitengo hiki kimefanya marekebisho katika maeneo mbalimbali, ikiwa ni pamoja na kutengeneza uzio huu unao saidia kupita mazuwaru bila kusababisha msongamano.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: