Mazaru ya Hamza ya mashariki ni moja ya vituo vya mazuwaru wa Arubaini

Maoni katika picha
Idadi kubwa ya mazuwaru wa Arubaini wanaokuja kutoka mikoa ya kusini kumzuru Imamu Hussein na ndugu yake Abulfadhil Abbasi (a.s), hupitia katika mazaru ya Sayyid Ahmadi Gharifi anaye julikana kwa jina la Hamza Sharqiy iliyopo umbali wa kilometa (30) kusini ya mji wa Diwaniyya.

Kwa miaka mingi mazuwaru wamezowea kupita kwa Sayyid huyu kumpa pole ya msiba wa babu yake Imamu Hussein (a.s) na watu wa nyumbani kwake na wafuasi wake, pia hufanya kama kituo chao cha kupumzika, kwani mazaru ipo katika barabara inayotumiwa na mazuwaru, wanapo fika hapo wanafanya ziara, wanaswali na kupumzika, watumishi wa mazaru hiyo hushindana katika kuwahudumia, pamoja na wakazi wa mji huo, wanajulikana kwa ukarimu na mapenzi yao kwa maimamu wa Ahlulbait (a.s), utawakuta watoto kwa wakubwa, wanawake kwa wanaume wanashindana kuhudumia mazuwaru kwa kuwapa chakula, vinywaji mavazi na vinginevyo, kupitia mawakibu za kutoa huduma au katika nyumba zao ambazo wamefungua milango kwa ajili ya kuwahudumia mazuwaru tabia ambayo wameirithi kwa mababu na mababu.

Mpiga picha wa mtandao wa Alkafeel alikuwepo katika matembezi ya Arubaini na anakuletea baadhi ya picha za matembezi hayo.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: