Tambua utukufu na masharti ya ziara ya Arubaini

Maoni katika picha
Mwakilishi wa Marjaa Dini mkuu Mheshimiwa Shekh Abdulmahdi Karbalai katika khutuba ya kwanza ya swala ya Ijumaa tukufu (12 Safar 1441h) sawa na (11 Oktoba 2019m) amezungumzia utukufu na misingi ya ziara ya Arubaini ya Imamu Hussein (a.s), amesema kua:

Tunaishi katika kumbukumbu ya Arubaini ya Imamu Hussein (a.s) na matembezi ya mamilioni ya watu miongoni mwa wafuasi wake kutoka kila sehemu ya dunia wanao kuja kufanya ziara kwa Imamu Hussein (a.s), kuna hadithi kutoka kwa Imamu Swadiq (a.s) kuhusu utukufu wa kutembea kwenda kumzuru Imamu Hussein (a.s), iliyo pokewa na Shekh ibun Quluwaihi katika kitabu cha Kaamil Ziyaraat kutoka kwa Imamu Swadiq (a.s) anasema: (Atakaye ondoka nyumbani kwake kwa ajili ya kwenda kuzuru kaburi la Hussein bun Ali –a.s- akiwa anatembea, Mwenyezi Mungu atamwandikia thawabu na atamfutia dhambi kwa kila hatua, hadi atakapofika katika jengo la kaburi Mwenyezi Mungu humwandika katika walio faulu, na anapo maliza ibada zake Mwenyezi Mungu humwandika katika walio fuzu, anapotaka kuondoka huja malaika na kumwambia: Hakika Mtume mtukufu anakutolea salam na anakuambia fanya mambo mema hakika Mwenyezi Mungu amekusamehe makosa yaliyo pita).

Lazima tuzingatie utukufu huu mkubwa, na nafasi ya pekee aliyo nayo zaairu wa Imamu Hussein (a.s) anaye kwenda kwa miguu, miongoni mwa mambo muhimu ya kuzingatiwa ni:

  • - Ili tuwe miongoni mwa mazuwaru wa Arubaini lazima tujue umuhimu wake na sababu za Mwenyezi Mungu na Mtume wake pamoja na maimamu kuihimiza na ukubwa wa thawabu zake.
  • - Hakika sababu ya kuhimizwa ziara ya Imamu Hussein na malalo zingine za Maimamu (a.s) ni kwa sababu walikua mfano mwema katika kumtii Mwenyezi Mungu na kupigana jihadi kwa ajili ya Dini yake, na wao ni mfano mkubwa katika kufuata sheria zake, kipindi cha ziara ni fursa ya kuimarisha uhusiano kati ya mja na muumba wake na kupambika na maadili mema.
  • - Miongoni mwa masharti muhimu ya ziara ni kufanya toba ya kweli na kuacha madhambi, pamoja na kuisafisha nafsi na mambo mabaya sambamba na kujiepusha na ria, migogoro na kuwa na maendeleo mazuri baada ya ziara ya Arubaini.
  • - Miongoni mwa alama za kuimarisha uhusiano na Mwenyezi Mungu mtukufu katika msimu wa ziara ya Arubaini ni kuswali mwanzoni mwa wakati wake, Imamu Hussein (a.s) aliswali katikati ya vita nayo ndio ibada ubwa zaidi mbele ya Mwenyezi Mungu mtukufu.
  • - Inatakiwa kufaidika na ziara hii kwa kujifunza mambo ya kifiqhi na aqida kwa mubalighina waliopo barabarani, pia inatakiwa kuacha utesi, uongo, matusi na kuudhi watu.
  • - Kipindi cha ziara ya Arubaini ni kipindi cha kutakasa roho na kurekebisha tabia, lazima kulinda haki za watu, kuna mazuwaru kutoka mataifa mbalimbali yatupasa kuwapokea na kuwahudumia kwa adabu kubwa.
  • - Yatupasa kuchunga heshima ya barabara na kuheshimu utaratibu wa kila mahala hadi ndani ya Ataba tukufu kwa ajili ya kulinda usalama wa mazuwaru watukufu.
  • - Usia wa mwisho unahusu wanawake wanaokuja ziara wanatakiwa kulinda hijabu na kujiepusha na mchanganyiko usio kubalika kisheria, wajifunze kutoka kwa bibi Zainabu (a.s).
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: