Sayyid Sistani: Watu wote wanatakiwa kushirikiana katika kuratibu ziara hii tukufu na kuhakikisha amani na usalama kwa mazuwaru

Maoni katika picha
Miongoni mwa maswali yaliyo elekezwa katika ofisi ya Marjaa Dini mkuu Sayyid Husseini Sistani kuhusu baadhi ya mambo yanayo husiana na usafi katika barabara zinazo tumiwa na mazuwaru wa Arubaini, moja ya maswali hayo ni:

Kwa jina la Mwenyezi Mungu mwingi wa rehema mwenye kurehemu

Asalamu alaikum wa rahmatullahi wa barakaatuhu.. kutokana na kukaribia kwa ziara tukufu ya Arubaini, tunapenda kuuliza mambo yanayo husiana na usafi kwenye barabara zinazo tumiwa na mazuwaru, baada ya kuwa na mamilioni ya mazuwaru na ugumu wa kusimamia usafi kwa mtu mmoja mmoja, changamoto hii ipo wazi.. je unaweza kutupa nasaha sisi na wahudumu wa mawakibu pamoja na mazuwaru kuhusu kutunza usafi na kua na utaratibu mzuri wa kuwahudumia mazuwaru wa Imamu Hussein (a.s)?

Jibu la ofisi ya Mheshimiwa Marjaa Dini mkuu lilikua kama ifuatavyo: Kila mtu anatakiwa kutunza usafi, hakika usafi ni katika Imani –kama ilivyo pokewa katika hadithi tukufu-, inatakiwa kutoa ushirikiano katika kuratibu ziara hii na kulinda amani ya mazuwaru, bila shaka ziara itakua na muonekano mzuri kama itasifika kwa usafi na mpangilio mzuri, pamoja na adabu nzuri ya mazuwaru, tunamuomba Mwenyezi Mungu awawafikishe watu wote kufuata utaratibu mzuri na awakubalie ibada zao hakika yeye ni mkuu wa kufanikisha.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: