Bado Atabatu Abbasiyya tukufu inaendelea kufundisha usomaji sahihi wa Qur’ani kwenye ziara ya Arubaini, Maahadi ya Qur’ani imefungua maonyesho ya Qur’ani na vituo vya kusomesha usomaji sahihi wa Qur’ani katika mradi wa tabligh huko Najafu.
Maonyesho hayo yanahusisha mabango yanayo onyesha mafundisho muhimu ya Qur’ani na maelekezo ya Marjaa Dini mkuu yanayo himiza kushikamana na Qur’ani tukufu na kizazi kitakasifu pamoja na kufanyia kazi hukumu za kitabu cha Mwenyezi Mungu na kukifanya kua ndio muongozo wa maisha yetu ya kila siku, zimeonyeshwa pia harakati zinazo fanywa na Maahadi ya Qur’ani katika mji wa Karbala na mikoa mingine, kama sehemu ya kuwahamasisha waweze kunufaika nayo.
Maahadi ya Qur’ani tukufu chini ya Atabatu Abbasiyya, imechukua jukumu la kufundisha Qur’ani tukufu, inashiriki katika vituo vilivyopo kwenye barabara zinazo tumiwa na wapenzi wa Imamu Hussein (a.s) -kwenda Karbala-, wanafundisha usomaji sahihi wa Qur’ani tukufu hasa kwa wageni wasio fahamu kiarabu, kuna walimu walio bobea wenye uwezo mkubwa wa kufundisha matamshi sahihi ya herufi za Qur’ani kwa njia rahisi, hakika hii ni fursa muhimu.
Fahamu vituo hivyo vinafundisha mambo mbalimbali yanayo husu Qur’ani, na vimeenea barabara zote kuu zinazo elekea Karbala kwa bwana wa mashahidi (a.s).