Hawa hapa watu wa kusini mwa Iraq, tangu ulipo ingia mwezi wa Safar wamefungua milango yao na kutoa huduma kwa kila mtu anayekwenda Karbala, wanagawa vyakula na vinywaji, kuwahudumia mazuwaru wa Imamu Hussein (a.s) ndio utamaduni wao, utamaduni huo wa ukaribu upo ndani ya damu zao, hakika ni watu wa kupigiwa mfano.
Ukaribu wao ni wa hali ya juu kabisa yaani hauelezeki, mgahawa wa Sayyid Hasuun Daraji katika wilaya ya Warkaa mkoa wa Muthanna ni moja ya vielelezo vya ukarimu wao, katika siku za ziara ya Arubaini mgahawa huo hubadilika na kua sehemu ya kuwahudumia mazuwaru wa Arubaini wanao pita kuelekea Karbala kwa Imamu Hussein na ndugu yake Abulfadhil Abbasi (a.s), katika mgahawa huo mazuwaru hupewa chakula, vinywaji na malazi, hakika mgahawa huo ni kielelezo cha ukarimu na ushujaa, hufanya hivyo kila mwaka na hukamilisha kazi zao kwa kwenda kuungana na Hussein (a.s).
Kumbuka kua wakazi wa wilaya ya Warkaa na mkoa mzima wa Muthanna walianza mapema kutoa huduma kwa mazuwaru wanaokwenda Karbala kwa baba wa watu huru (a.s), na maelfu ya vijana wa mji huo wameungana na wenzao katika misafara ya kwenda Karbala kufanya ziara ya Arubaini ya Imamu Hussein (a.s).