Sayyid Sistani aongea na mazuwaru wa Imamu Hussein (a.s): Allah Allah stara na hijabu

Maoni katika picha
Miongoni mwa maelekezo na usia unaotolewa na ofisi ya Mheshimiwa Marjaa Dini mkuu Ayatullah Sayyid Ali Hussein Sistani kwa mazuwaru wa Arubaini ya Imamu Hussein (a.s), jambo alilo sisitiza ni stara na hijabu, hakika hilo ni miongoni mwa mambo muhimu waliyo pambika nayo Ahlulbait (a.s), hadi katika siku ngumu zaidi ya vita ya Karbala, walikua mfano wa kuigwa katika kujistiri, aliyasema hayo wakati akijibu swali kutoka kwa mazuwaru walio omba nasaha za ubaba kuhusu tukio hili, kwenye mtandao ramsi wa ofisi ya Mheshimiwa Marjaa Dini mkuu imeandikwa nakala hii:

(Allah Allah stara na hijabu, hakika ni jambo muhimu walilo pambika nalo Ahlulbait (a.s) hata walipo kua katika mazingira magumu zaidi katika vita ya Karbala, walikua mfano wa kuigwa katika kujistiri, njama za maadui zao hazikuwafanya wavunje heshima zao kwa watu, mazuwaru wote –hasa waislamu- yawapasa kujistiri na kuchunga hijabu na mavazi yao, wajiepushe kuvaa nguo zinazo punguza heshima ya hijabu kama vile nguo za kubana, kuchanganyika na wanaume kusiko kubalika kisheria na kujipamba mapambo yasiyo faa, wanatakiwa kua wanyenyekevu na kulinda heshima ya ziara hii tukufu).
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: