Kitengo cha maadhimisho na mawakibu Husseiniyya katika Ataba mbili tukufu kimetangaza kua: Idadi ya mawakibu zinazotoa huduma kwa mazuwaru wa Arubani wanaopita kwenye eneo la mkoa wa Dhiqaar imefika (3422) zilizo sajiliwa rasmi, bado kuna mamia ya Husseiniyya na nyuma za watu binafsi pamoja na mawakibu zingine ambazo hazijasajiliwa rasmi na zinatoa kuduma kwa mazuwaru tangu siku ya kwanza, maukibu hizo zimeenea kila sehemu katika eneo la mkoa huo.
Akaongeza kua: “Kuna mawakibu zingine za wakazi wa mkoa huu zimeenda kutoa huduma kwenye mikoa ningine inayo pitiwa na mazuwaru, sambamba na watu wengine kushiriki kwenye mawakibu za watu wa mikoa mingine ndani ya mkoa mtukufu wa Karbala na kwenye barabara zinazo elekea Karbala”.
Akabainisha kua: “Hakika mawakibu za kutoa huduma, haziishii kutoa huduma ya chakula na vinywaji peke yake, zina mchango mkubwa katika kushirikiana na vyombo vya ulinzi na usalama kuhakikisha amani inatawala, baada ya kuisha misafara ya mazuwaru katika mkoa huu, wahudumu wa mawakibu hizo wataenda kufanya ziara Karbala kwa miguu ili wapate utukufu mara mbili wa kutoa huduma na kufanya ziara”.