Baada ya kuingia asubuhi ya (16 Safar 1441h) sawa na (15 Oktoba 2019m), mawakibu za kuomboleza (zanjiil) zimeanza kumiminika katika malalo ya Imamu Hussein na ndugu yake Abulfadhil Abbasi (a.s) kutoka mikoa tofauti ya Iraq, wanakuja kutoa pole na kuomboleza Arubaini ya Imamu Hussein (a.s).
Mawakibu hizo zinaingia kwa kufuata ratiba iliyo pangwa na kitengo cha maadhimisho na mawakibu Husseiniyya chini ya Ataba mbili Husseiniyya na Abbasiyya, watumishi wa kitengo hicho pamoja na kitengo cha kulinda nidham na wafanyakazi wa kujitolea, wameshiriki katika mawakibu hizo.
Matembezi ya mawakibu yameratibiwa vizuri ndani ya haram hizo na katika uwanja wa katikati ya haram mbili kwa namna ambayo hayatatizi harakati za mazuwaru wanao endelea kuongezeka kila siku.
Matembezi ya mawakibu yalianzia barabara ya Kibla ya Imamu Hussein (a.s) hadi katika uwanja wa haram yake tukufu, kisha zikaenda katika malalo ya Abulfadhil Abbasi (a.s) kwa kupitia eneo la katikati ya haram mbili tukufu, huku wanaimba kaswida za kuomboleza.
Mawakibu za zanjiil huwa ni mistari miwili mirefu, hutembea pembezoni mwa barabara huku katikati yao kukiwa na vijana walio beba bendera, halafu huwa wanapiga mdundo wa ngoma na kujipiga zanjeel migongoni kwa imani ya hali ya juu, mazuwaru watukufu husimama pembeni ya barabara na kuangalia nanma mawakibu za watu waliojaa imani kwa Ahlulbait (a.s) zinavyo pita.