Kwa ajili ya kuratibu matembezi ya mazuwaru wanao ingia katika haram ya Abulfadhil Abbasi (a.s), Atabatu Abbasiyya tukufu kupitia idara ya sauti (vipaza sauti) imeweka vipaza sauti kwenye uzio wa haram tukufu, vinavyo tumika kutangaza maelekezo mbalimbali kwa mazuwaru, matangazo hayo yanasikika hadi mbali, ili kumuwezesha zaairu kutambua mambo anayo takiwa kufanya kabla hajaingia ndani ya haram tukufu.
Vipaza sauti hivyo vimeunganishwa na chumba kikuu cha vipaza sauti vya Atabatu Abbasiyya kilichopo ndani ya haram tukufu, maelekezo tofauti yanatolewa kwa mazuwaru kabla hawajaingia ndani ya haram tukufu ya Abulfadhil Abbasi (a.s), kuhusu adabu za ziara, umuhimu wa kuweka viatu kwenye mabanda maalum ya kutunzia viatu, kuweka simu na vifaa vingine katika mabanda ya Amanaat, unapo ingia wakati wa swala yanatowa baadhi ya mafundisho ya Dini kutoka kwenye haram mbili tukufu yanayo fuatiwa na kisomo cha Quráni kisha adhana na swala.
Matangazo na maelekezo hayo yanatolewa saa ishirini na nne kwa lugha zaidi ya moja, kutokana na wingi wa mataifa pamoja na lugha za mazuwaru wanaokuja kufanya ziara ya arubaini ya Imamu Hussein (a.s) kutoka kila sehemu ya dunia.
Tambua kua Atabatu Abbasiyya tukufu kupitia vitengo na idara zake inajitahidi kuhakikisha ziara inafanyika katika mazingira mazuri, na mafanikio yanaendelea mwaka baada ya mwaka.