Katibu mkuu wa Atabatu Radhawiyya tukufu Hujjat Islaam Shekh Ahmadi Marwi na wajumbe alio fuatana nao wapo katika mgahawa wa Atabatu Abbasiyya wa nje uliopo barabara ya (Najafu / Karbala), na amekutana na Mheshimiwa kiongozi mkuu wa kisheria wa Atabatu Abbasiyya Mheshimiwa Sayyid Ahmadi Swafi na katibu mkuu Mhandisi Muhammad Ashiqar pamoja na wajumbe wa kamati kuu ya uongozi, jioni ya Jumatatu (15 Safar 1441h) sawa na (14 Oktoba 2019m).
Mheshimiwa Sayyid Ahmadi Swafi amewakaribisha wageni na kuwatakia mafanikio mema na kukubaliwa ibada zao, ameonyesha kufurahishwa na ugeni huo mtukufu katika haram ya Abulfadhil (a.s).
Naye Mheshimiwa Shekh Ahmadi Marwi amepongeza kazi nzuri zinazo fanywa na Atabatu Abbasiyya tukufu inayo shuhudia maendeleo katika sekta ya ujenzi na utowaji wa huduma.