Kitengo cha maadhimisho na mawakibu Husseiniyya: Maukibu za kutoa huduma zimefika zaidi ya (1200) katika mkoa wa Muthanna huku nyingine nyingi zikitoa huduma katika mkoa wa Karbala

Maoni katika picha
Kitengo cha miradi na mawakibu Husseiniyya katika Ataba mbili tukufu kimetangaza kua: “Mawakibu zilizo toa huduma kwa mazuwaru wa Arubaini waliopita katika mkuo wa Muthanna mwaka huu zilizo sajiliwa rasmi ni (1227), bila kuhesabu mamia ya Husseiniyya na nyumba za makazi ya watu pamoja na mawakibu ambazo hazikusajiliwa zilizo anza kuhudumia mazuwaru tangu siku ya kwanza ambayo mazuwaru walianza kuingia katika mji huo”.

Akaongeza kua: “Kuna mawakibu za watu wa Muthanna ambazo zinatoa huduma kwenye mikoa mingine ambayo inapitiwa na mazuwaru, huku zingine zikitoa huduma katika mkoa wa Karbala”.

Akabainisha kua: “Mawakibu za kutoa huduma haziishii kugawa chakula na vinywaji peke yake, bali zina mchango mkubwa wa kuimarisha ulinzi na usalama kwa kushirikiana na vyombo vya usalama, baada ya kuisha misafara ya mazuwaru katika mkoa huo, watumishi wa mawakibu za kutoa huduma huanza safazi za kwenda Karbala kufanya ziara”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: