Kutoka Ujerumani: Maandalizi ya kushiriki kwa Atabatu Abbasiyya tukufu kwenye maonyesho ya vitabu ya kimataifa yatakayo fanyika mjini Frankfud yamekamilika

Maoni katika picha
Kusambaza utamaduni wa uadilifu na kutambulisha misingi ya uislamu halisi ulio fundishwa na Mtume Muhammad (a.s) ndio malengo makuu ya kushiriki kwa Atabatu Abbasiyya tukufu katika maonyesho ya kimataifa ya (82) yatakayo fanyika mjini Frankfud.

Sayyid Ahmadi Radhi Husseini muwakilishi wa Atabatu Abbasiyya huko Ulaya amesema kua: “Hii ni mara ya pili Atabatu Abbasiyya tukufu inashiriki katika maonyesho haya ikiwa na aina (200) za vitabu na machapisho yake”.

Akafafanua kua: “Tumekamilisha maandalizi ya kushiriki kwenye maonyesho hayo, na tumeandaa faharasi ya machapisho yatakayo onyeshwa kwa ajili ya kumrahisishia mtu atakaetembelea maonyesho hayo”.

Kumbuka kua Atabatu Abbasiyya tukufu imesha shiriki mara nyingi katika maonyesho ya kimataifa na makongamano ndani na nje ya Iraq, kote hufanya kazi ya kusambaza fikra na mafundisho ya Ahlulbait (a.s), tawi lake hupata muitikio mkubwa katika kila maonyesho, nayo hujitahidi kuongeza machapisho kwenye kila maonyesho.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: