Miongoni mwa kazi zinazo fanywa na kitengo hicho kwa mujibu wa maelezo ya Sayyid Mussawi ni:
- - Kuweka waelekezaji katika eneo la uwanja wa katikati ya haram mbili na maeneo yanayo zunguka malalo mbili tukufu kwa ajili ya kuongoza mazuwaru na kuwaelekeza sehemu wanazo hitaji.
- - Kuweka mageti ya muda yanayo hamishika kwa ajili ya kukagua mazuwaru na mawakibu.
- - Kuratibu uingiaji na utokaji wa mazuwaru na mawakibu katika haram mbili tukufu.
- - Kutenga sehemu maalum ya kupumzika wanawake na sehem ya wanaume kwa ajili ya kuondoa mchanganyiko usio faa baina yao.
- - Kuratibu uingiaji na utokaji wa vifaa vya usafiri katika eneo la katikati ya haram mbili.
Akabainisha kua: “Kazi zote hizo zinafanywa na watumishi wa idara hiyo pamoja na wafanyakazi wa kujitolea, wanafanya kazi usiku na mchana”.