Miongoni mwa maelekezo na usia uliotolewa na ofisi ya Mheshimiwa Marjaa Dini mkuu Sayyid Ali Husseini Sistani kwa watu wanaokwenda kufanya ziara ya Arubaini ya Imamu Hussein (a.s) ni Ikhlasi, kwa sababu thamani ya ibada ya mwanaadamu ni Ikhlasi yake kwa Mwenyezi Mungu mtukufu, kwani Allah hakubali ibada ispokua iliyo fanywa kwa Ikhlasi, aliyasema hayo wakati akijibu swali kutoka kwa waumini walio omba nasaha zake, nakala ifuatayo imeandikwa kwenye mtandao rasmi wa ofisi yake:
Allah Allah katika Ikhlasi, hakika thamani ya ibada inatokana na Ikhlasi yake kwa Mwenyezi Mungu, Alla hakubali ibada ispokua iliyo fanywa kwa Ikhlasi, imepokewa kutoka kwa Mtume (s.a.w.w) wakati waislamu wanahama kwenda Madina alisema kua: (Yule ambaye amehama kwa ajili ya Mwenyezi Mungu na Mtume wake, basi kuhama kwake ni kwa ajili yao, na aliyehama kwa ajili ya dunia, basi kuhama kwake ni kwa sababu ya dunia, hakika Mwenyezi Mungu huongeza malipo ya mja wake hadi mia saba na humuongeza zaidi amtakae).
Mazuwaru wanatakiwa kumtaja Mwenyezi Mungu wakati wa matembezi yao na wajipambe na Ikhlasi katika kila kitu, watambue kua Mwenyezi Mungu mtukufu hajawahi kumpa mje wane neema kubwa zaidi ya Ikhlasi, ibada yeyote bila Iklasi hupotea, na ibada yenye Ikhlasi hudumu milele duniani na akhera.