Shirika la kuzalisha wanyama na chakula Nuurul-Kafeel: Halijaongeza bei za bidhaa zake katika kipindi cha ziara ya Arubaini bali watu wa mawakibu wanauziwa kwa bei ya punguzo

Maoni katika picha
Shirika la kuzalisha wanyama na chakula Nuurul-Kafeel chini ya Atabatu Abbasiyya tukufu limesema kua halijaongeza bei katika bidhaa zake wakati huu wa ziara ya Arubaini, kuanzia makao yake makuu katika mkoa wa Karbala hadi kwenye vituo vyake vya mauzo vilivyopo mikoani vipatavyo (213), bali mawakibu za kutoa huduma zinauziwa kwa bei ya punguzo kwa ajili ya kuzisaidia ziweze kutoa huduma bora kwa mazuwaru.

Shirika linatoa wito kwa wananchi na viongozi wa mawakibu watakao pandishiwa bei au kufanyiwa hujuma yeyote wawasiliane na nasi kwa namba za simu zifuatayo (07801966624), au namba ya masoko (07801966622), au namba ya ofisi ya Najafu (07800789053), au ofisi ya Basra namba (00964 (0) 7713141624) au unaweza kutuandikia barua pepe kwa anuani ifuatayo hp@islamicalkafeel.com au kupitia mtandao wetu maalum: http://www.nooralkafeel.com.

Kumbuka kua shirika limejiandaa kuingiza sokoni bidhaa zote zinazo hitajiwa na mawakibu za kutoa huduma, na kutoa ushindani mkubwa kwa wafanya biashara ambao hutumia kipindi hiki kuongeza bei za bidhaa, shirika limeweka shehena kubwa ya bidhaa katika vituo vyake vya mauzo vyote vilivyopo ndani na nje ya mkoa wa Karbala.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: