Mgahawa wa Abulfadhil Abbasi (a.s) umegawa zaidi ya sahani milioni moja za chakula ndani ya siku kumi na bado unaendelea kugawa

Maoni katika picha
Kitengo cha mgahawa wa Atabatu Abbasiyya kimetangaza kua zaidi ya sahani za chakula milioni moja zimesha tolewa kwa mazuwaru wa Arubaini ndani ya siku kumi pekee, na bado unaendelea kutoa huduma za chakula kutipia vituo ilivyo fungua na kwa kufuata utaratibu maalum.

Kitengo kimebainisha kua mwaka huu kilianza mapema kutoa huduma ya chakula kutokana na kuongezeka kwa idadi ya mazuwaru kutoka nje ya Iraq na kutokuwepo mawakibu za kutoa huduma wakati huo, ndipo mgahawa ukachukua jukumu la kugawa chakula kwa mazuwaru na utaendelea kugawa hadi kilele cha ziara hii na baada ya ziara, wao wataendelea kugawa chakula baada ya mawakibu zingine kuaondoka, mgahawa wa Abulfadhil Abbasi ni wa kwanza katika kutoa huduma na wa mwisho katika kufunga huduma.

Fahamu kua unatoa vyakula vya aina mbalimbali katika milo mitatu, inatumia madirisha manne kugawa chakula, matatu yapo nje ya haram na moja lipo ndani ya haram kwenye ukumbi wa mgahawa.

Vitengo vyote vya Atabatu Abbasiyya tukufu vimejipanga kutoa huduma bora wakati wa ziara ya Arubaini, kila kitengo kinafanya juhudi kubwa katuka kuwahudumia mazuwaru wa Arubaini ya Imamu Hussein (a.s).
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: