Kitengo cha maadhimisho na mawakibu Husseiniyya chatoa ratiba ya kuingia kwa mawakibu za kuomboleza (matam)

Maoni katika picha
Kitengo cha maadhimisho na vikundi vya Husseiniyya chini ya Ataba mbili tukufu Husseiniyya na Abbasiyya, kinacho husika na kuratibu uingiaji wa mawakibu na vikundi vya Husseiniyya, kimeandaa ratiba maalum ya kuingia mawakibu za kuomboleza (matam) zinazo shiriki katika Arubaini ya Imamu Hussein (a.s).

Kitengo kinawataka wasimamizi wote wa mawakibu na vikundi vya Huseiniyya waheshimu muda uliopangwa, muda huo ni kuanzia mwanzo kabisa wa matembezi kwenye sehemu iliyopo barabara ya Kibla ya Imamu Hussein (a.s) kisha kuingia katika Atabatu Husseiniyya tukufu halafu kuelekea katika Atabatu Abbasiyya hadi mwisho wa matembezi, tunatarajia ratiba hiyo itekelezwe kama ilivyo pangwa kwa ajili ya kumtumikia Imamu Hussein (a.s).

18 Safar 1441h

Mkoa wa Dhiqaar wilaya na vitongoji vyake kuanzia saa 12 asubuhi hadi saa 3 asubuhi.

Mkoa wa misaan wilaya na vitongoji vyake kuanzia saa 3 asubuhi hadi saa 5 kabla ya Adhuhuri.

Maukibu ya kuomboleza ya kamati kuu na taasisi ya Badru kuanzia saa 7 Adhuhuri hadi saa 8 baada ya Adhuhuri.

Mkoa wa Diyala na Swalahu Dini kuanzia saa 8 baada ya Adhuhuri hadi saa 10 Alasiri.

Chama cha Answaaru Shahiid Swadri kuanzia saa 10 Alasiri hadi saa 11:30 jioni.

Mkoa wa Waasit wilaya na vitongoji vyake kuanzia saa 12:30 usiku hadi saa 2 usiku.

Mkoa wa Qadisiyya wilaya na vitongoji vyake kuanzia saa 2 usiku hadi saa 4 usiku.

Mkoa wa Bagdad wilaya na vitongoji vyake kuanzia saa 4 usiku hadi saa 5 usiku.

Maukibu kutoka nchi za kiarabu na kiislamu kuanzia saa 5 usiku hadi saa 6 usiku.

19 Safar 1441h

Maukibu za Kadhimiyya tukufu kuanzia saa 1 asubuhi hadi saa 2 asubuhi.

Mkoa wa Najafu wilaya na vitongoji vyake kuanzia saa 2 asubuhi hadi saa 3 asubuhi.

Mkoa wa Basra kuanzia saa 3 asubuhi hadi saa 5 kabla ya Adhuhuri.

Mkoa wa Muthanna kuanzia saa 7 Adhuhuri hadi saa 8 Adhuhuri.

Maukibu ya Hizbu da’awah (kabila la bani tamim) kuanzia saa 8 Adhuhuri hadi saa 10 Alasiri.

Mkoa wa Baabil wilaya na viyongoji vwake kuanzia saa 10 alasiri hadi saa 11:30 alasiri.

Mkoa wa Karkuuk na Nainawa kuanzia saa 1 usiku hadi saa 3 usiku.

Wilaya ya Ainu-Tamru / Karbala kuanzia saa 3 usiku hadi saa 4 usiku.

Maukibu za nchi za kiarabu na kiislamu kuanzia saa 4 usiku hadi saa 6 Usiku.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: