(Tunajifunza Twafu) ni anuani ya filamu inayo angaliwa kila siku na zaidi ya watoto 40 waliokuja na wazazi wao kumzuru Imamu Hussein (a.s) katika kumbukumbu ya Arubaini

Maoni katika picha
Katika kueneza utamaduni utokanao na fikra za Imamu Hussein (a.s) za kupinga uvunjifu wa misingi ya ubinaadamu, ukizingatia kua mtoto ni nguzo muhimu ya mwanadamu na takiwa kupewa misingi ya ubinaadamu, ofisi ya wanawake katika Atabatu Abbasiyya tukufu imetenga nafasi ya watoto kwenye hema lake.

Wanaonyesha filamu ya katuni fupi fupi katika moja ya kumbi za maukibu ya Ummul Banina (a.s) zinazo fundisha misingi ya ubinaadamu kutokana na vita ya Twafu, filamu hiyo imeandaliwa na Aalaau Muhammad Hussein Khafaaf kutoka idara ya kusaidia usomaji katika ofisi ya wanawake, ameuambia mtandao wa Alkafeel ku: “Ili kuwafanya watoto wawe na tabia nzuri wanahitaji mafundisho yatokanayo na vitu vya kuvutia, ili waweze kuathirika katika akili zao, kwa hiyo wanapewa mafundisho kwa kutumia filamu kisha wanapewa mawaidha elekezi”.

Program hiyo inahudhuriwa na watoto kutoka ndani na nje ya Iraq, wameonyesha kufurahishwa sana na filamu, tumeongea na mtoto Muhammad Sayyid Kaadhim ambaye anamsaidia mzazi wake katika maukibu ya kutoa huduma, amesema kua: “Katika filamu nimesoma umuhimu wa usafi, filamu ilikua nzuri sana natamani niiangalie tena”. Mtoto mwingine aitwaye Zainabu kutoka Kufa akasema: “Katika filamu hii nimejifunza kua Imamu Hussein (a.s) aliwapa umuhimu watoto na alikua anawapenda”. Naye Maryam kutoka Iran akasema: “Nimeelewa yaliyo kua yakionyeshwa katika filamu japokua ipo kwa kiarabu”.

Wazazi wa watoto wamepongeza program hii na wamesema kua inatoa picha mpya katika mafundisho ya Husseiniyya, huku wakisema kwa sauti (Shukran yaa Hussein) na (Labbaika yaa Hussein) kuonyesha mapenzi yao kwa Imamu Hussein (a.s).
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: