kwa mujibu wa maelezo ya Sayyid Hashim Mussawi, akaongeza kusema kua: “Tulianza mapema kujiandaa na ziara hii, tuliongeza uwezo wa uzalishaji wa kiwanda na tukaandaa vifaa vyote kabla ya kuanza msimu wa ziara, uzalishaji ulikua haukidhi haja, tumefanikiwa kuandaa hazina kubwa ya barafu, kipindi hiki cha ziara tumeweza kugawa barafu sehemu mbalimbali”.
Akaongeza kua: “Miongoni mwa sehemu tunazo gawa barafu ni:
- - Mawakibu za kutoa huduma zilizo sambaa katika barabara zinazo elekea Karbala kwa ajili ya kupoza maji, juisi na vinyaji vingine sambamba na baadhi ya vyakula.
- - Majengo ya kutoa huduma na miji ya mazuwaru iliyo chini ya Atabatu Abbasiyya tukufu.
- - Atabatu Abbasiyya tukufu na vitengo vyake ikiwemo haram tukufu na maeneo jirani.
- - Vyombo vya ulinzi na usalama vilivyopo Karbala na maeneo ya mpakani na Karbala.
- - Baadhi ya miji ya mazuwaru na vituo vya Atabatu Husseiniyya vilivyo karibu na kiwanda”.
Akasema: “Hali kadhalika tumewasha kituo cha kusafisha maji (RO) kwa ajili ya kugawa maji na barafu moja kwa moja au kwa kutumia gari maalum za kusambaza maji, kiwango cha uzalishaji kimefikia (ujazo wa mita 16) kwa saa na kinafanya kazi saa 24 kwa siku”.