Katika mkoa wa Baabil: Zaidi ya maukibu (2200) zimetoa huduma kwa mazuwaru wa Arubaini.

Maoni katika picha
Mkoa wa Baabil ni moja ya lango kuu linalo tumiwa na mazuwaru wanao kwenda Karbala tukufu katika ziara ya Arubaini, taarifa ya kitengo cha maadhimisho na mawakibu Husseiniyya inasema kua: “Idadi ya mawakibu zilizo toa huduma kwa mazuwaru katika eneo la mkoa wa Baabil ilifika (2256) ambazo zilisajiliwa rasmi, bado zile ambazo hazikusajiliwa pamoja na Husseiniyya na nyumba za makazi ya watu ambazo zimetoa huduma kwa mazuwaru tangu siku ya kwanza ambayo mazuwaru walianza kuingia katika mkoa huo”.

Wakafafanua kua: “Mawakibu zimeenea kwenye njia zote zinazo tumiwa na mazuwaru, huku barabara zenye mazuwaru wengi zikipewa kipaombele zaidi, pia kuna mawakibu zinazo toa huduma katika mkoa wa Karbala na kwenye barabara zingine zinazo elekea Karbala”.

Wakabainisha kua: “Mwaka huu harakati za mazuwaru wanao kwenda Karbala zimeanza mapema, mawakibu haziishii kutoa huduma za chakula na vinywaji peke yake, bali zinashirikiana na vyombo vya ulinzi na usalama katika kulinda amani, baada ya kuisha misafara ya mazuwaru katika mkoa huu, watumishi wa mawakibu wataenda kwa miguu Karbala kufanya ziara na kupata utukufu mara mbili, wa kutoa huduma kwa mazuwaru na kufanya ziara”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: