Sayyid Sistani awaombea kwa Mwenyezi Mungu mazuwaru wa Imamu Hussein (a.s) kukubali ziara zao kama anavyo wakubalia waja wake wema

Maoni katika picha
Ofini ya Marjaa Dini mkuu Ayatullah Sayyid Ali Husseini Sistani imetoa maelekezo mbalimbali kwa mazuwaru wa Arubaini ya Imamu Hussein (a.s), miongoni mwa maelekezo hayo ni: “Waumini waliokuja katika ziara hii tukufu yawapasa kutambua kua Mwenyezi Mungu ameleta Mitume na mawasii ili wawe kiigizo chema kwa watu waongoke kutokana na mafundisho yao na wafuate mwenendo wao”.

Mwenyezi Mungu amejaalia kutembelea malalo zao kua sehemu ya kuenzi utajo wao na mafundisho ya Mwenyezi Mungu, hakika wao walikua mfano mwema katika kumtii (s.w.t) kupigana jihadi na kujitolea kwa ajili ya Dni yake madhubuti.

Amehitimisha maelekezo yake kwa kuomba dua ifutayo: “Tunamuomba Mwenyezi Mungu mtukufu amuongezee utukufu Mtume Muhammad (s.a.w.w) na watu wa nyumbani kwake watakasifu (a.s) duniani na akhera kwa namna walivyo jitolea katika njia yake na wakapigana jihadi kwa ajili yake, awaongezee rehema na amani kama alivyo fanya kwa waja wema kabla yao hususan Ibrahim na kizazi cha Ibrahim, tunamuomba Mwenyezi Mungu mtukufu awabariki mazuwaru wa Abu Abdillahi Hussein (a.s) na awakubalie kama anavyo wakubalia waja wema, ziara yao hii iwe ni kigezo chema katika umri wao wote uliobaki, awalipe thawabu kutokana na utukufu wa watu wa nyumba ya Mtume (a.s), kutokana na mapenzi yao kwao na kufuata mwenendo wao pamoja na kusambaza ujumbe wao, awaite pamoja nao (a.s) siku ya kiyama atakapo itwa kila mtu na Imamu wake, na waliopata shahada wakiwa katika njia hii wafufuliwe pamoja na Hussein (a.s) na wafuasi wake kutokana na subira waliyo fanya itokanayo na mapenzi yao kwake, hakika Mwenyezi Mungu ni mwingi wa kusikia mwingi wa kujibu)..
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: