Marjaa Dini mkuu: Mazingatio ya kweli na uwelewa wa kina wa mafundisho ya bwana wa mashahidi (a.s) yanatosha kusafisha roho zetu kutokana na dhulma pamoja na tabia mbaya

Maoni katika picha
Marjaa Dini mkuu amesema kua mazingatio ya kweli na uwelewa wa kina wa mafundisho ya bwana wa mashahidi (a.s) yatosha kusafisha roho zetu kutokana na dhulma pamoja na tabia mbaya… ameyasema hayo katika khutuba ya pili ya swala ya Ijumaa leo (19 Safar 1441h) sawa na (18 Oktoba 2019m) iliyo swaliwa ndani ya haram ya Imamu Hussein (a.s) chini ya uimamu wa Mheshimiwa Sayyid Ahmadi Swafi, ifuatayo ni nakala ya khutuba hiyo:

Mabwana na mabibi.. bila shaka kuna faida katika swala la ziara ya Arubaini –kuna faida nyingi- kuna hali ya kujijenga kiroho na kuimarisha Imani zetu, fikra sahihi katika mtazamo sahihi hua na matokeo mema, bwana wa mashahidi (a.s) alikua na mtazamo wa islahi, alisema kua: (Mimi sijatoka kwa shari wala ukamanda wala kufanya ufisadi au dhulma, hakika nimetoka kwa ajili ya kutafuta islahi katika umma wa babu yangu, nataka kuamrisha mema na kukataza mabaya, atakaye kubali haki Mwenyezi Mungu ndio mwenye haki, na atakae kata nitafanya subira hadi Mwenyezi Mungu ahukumu baina yetu naye ni mbora wa mahakibu).

Hakika (a.s) alifanikisha alicho kitaka pamoja na uchache wa wafuasi wake na uovu wa watu wa zama zake, alifanikiwa kwa sababu alikua anajua anacho fanya yeye pamoja na wafuasi wake, Mwenyezi Mungu anasema: (Sema: Hii ndio njia yangu –ninalingania kwa Mwenyezi Mungu kwa kujua- mimi na wanao nifuata. Na ametakasika Mwenyezi Mungu! Wala mimi si katika washirikina), baswirah ni uwelewa wa kina na kujua hatima ya jambo, lengo na vipengele muhimu kuhusu jambo husika, sio rahisi kwa kila mtu, tunakaribia kumaliza ziara ya Arubaini, ni matarajio yetu kua tumekua wakweli wa mwenendo wake mtukufu, tumehuisha nafsi zetu kupitia kuhuisha maombolezo haya, tumezitendea haki kwa kutafakari mazuri yanayo patikana katika mafundisho ya Imamu Hussein (a.s).

Hakika mazingatio ya kweli na uwelewa wa kina wa mafundisho ya bwana wa mashahidi (a.s) yanatosha kusafisha roho zetu kutokana na dhulma pamoja na tabia mbaya.

Mwenyezi Mungu awalinde mazuwaru wote na taifa letu pamoja na mataifa mengine na kila aina ya ubaya, atuwezeshe kukamilisha ziara kwa amani na utulivu, na mwisho wa maombi yetu husema kila sifa njema anastahiki Mwenyezi Mungu Mola mlezi wa walimwengu na rehema na amani ziwe juu ya Mtume Muhammad na kizazi chake kitakasifu.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: