Rais wa kitengo cha mawakibu na vikundi vya Husseiniyya chini ya Ataba mbili tukufu bwana Riyadh Ni’mah Salmaan amesema kua: Idadi ya mawakibu za kutoa huduma na kuomboleza kutoka nchi za kiarabu na kiajemi zilizo shiriki katika ziara ya Arubaini ya Imamu Hussein (a.s) na kusajiliwa rasmi mwaka huu 1441h, zimefika (225).
Akaongeza kua: “Mawakibu za kuomboleza, kuna za (matam na zanjiil), na zingine zinatoa huduma kwa mazuwaru wa Imamu Hussein na ndugu yake Abulfadhil Abbasi (a.s), kwa kuwapa chakula, vinywaji na mengineyo”.
Akabainisha kua: “Mawakibu hizo zimetoka katika nchi za kiarabu na kiajemi zifuatazo: (Saudia – Kuwait – Baharain – Sirya – Lebanon – Yemen – Oman – India – Iran – Pakistan – Afughanistan – Tailendi – Uturuki – Adharbaijan – Ufaransa – Ujerumani – Swiden – Uingereza – Marekani – Holandi – Kenya – Tanzania)”.